Fundi magari (jina limehifadhiwa) akipaka rangi vipuli vya roli aina ya Scania ndani ya yadi namba 678 iliyopo Kurasini, Dar es Salaam |
MWANDISHI WA PANORAMA
Issac Abdallah, mmiliki wa yadi ya magari makubwa (maroli aina ya Scania) namba 678 (Customer Bonded Ware House) iliyoko barabara ya Kilwa, Kurasini ameanza kuweweseka.
Weweseko la Abdallah limekuja baada ya kuripotiwa kwa taarifa kuwa yadi hiyo namba 678, sambamba na kuhifadhi magari ambayo hajalipiwa ushuru, inatumika pia kama karakana ambamo mafundi magari wamekuwa wakifungua vipuli vya magari mapya na kuvipeleka kusikojulikana na kufunga vipuli chakavu.
Akizungumza kuhusu ajira za mafundi magari wanaodaiwa kufungua vifaa vipya na kufunga chakavu kwenye magari mapya yaliyo katika yadi yake hiyo, kibali alichopewa na TRA kumruhusu kufanya kazi za ufundi magari ndani ya yadi, aina ya magari yanayotengenezwa na aina ya matengenezo yanayofanyka, Abdallah aliporomosha kauli ambazo tunasita kuziripoti kwa sababu ya maadili huku akionya asifuatiliwe.
āWewe ni mwandishi wa habariā¦ā¦.. kwanini umeandika mambo yasiyokuhusu? Nani kakuruhusu uandike ā¦ā¦. Kwani wewe umekuwa TRA? Sisi tumeruhusiwa na TRA kufanya matengenezo ya magari tunayoagiza ndani ya yadi yetu, kwanini hujaenda kuwauliza? Alisema kwa ukali Abdallah.
Tangu wiki iliyopita, Mamlaka ya Mapato (TRA) ilipoulizwa kuhusu hilo imekuwa bubu ambapo Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo alipoombwa ushirikiano aliuliza sababu za afisa anayetafutwa na alipoelezwa kuwa lengo ni kumtaka ajibu au atoe ufafanuzi kuhusu tuhuma kadhaa zinazoelekezwa yadi namba 678, hakutoa ushirikiano.
Richard Kayombo |
Tanzania PANORAMA imemtafuta bila mafanikio Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ili kuzunguzia suala hilo baada ya mamlaka zilizo chini yake kushindwa kutekeleza wajibu wake na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.
Awali, Tanzania PANORAMA iliripoti kuwapo hofu ya wizi wa vipuli vya magari katika yadi ya magari makubwa namba 678, (Customer Bonded Ware House) iliyoko barabara ya Kilwa, Kurasini ambayo sambamba na kuhifadhi magari ambayo hajalipiwa kodi imekuwa ikitumika kama karakana.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mafundi magari wanaohusika kuondoa vipuli katika magari yaliyo ndani ya yadi hiyo na kuvipeleka kusikojulikana kisha kuleta vingine chakavu wanatekeleza kazi hiyo kwa maelekezo ya Issac Abdallah.
Inadaiwa kuwa vifaa vinavyoondolewa katika magari hayo hupelekwa kuuzwa katika maduka ya vipuli vya magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kariakoo, kwenye magereji na kwa baadhi ya wenye magari makubwa ambao wanahitaji kubadili vipuli vilivyotumika kwenye magari yao kwa muda mrefu.
Kwamba, mafundi hao ambao huuza vipuli hivyo kwa bei kubwa, hununua vipuli vingine vilivyotumika muda mrefu kwa bei ya chini katika eneo la Gerezani Kariakoo na kwenda kuvifunga katika magari waliyotoa vipuli vipya.
Ā āKinachofanyika ni sawasawa na wizi kwa sababu hawa mafundi ambao Issac ndiye anayewaleta huwa wanakuja kufungua āspareā mpya kwenye magari mapya ambayo yanahifadhiwa hapa kabla ya kulipiwa kodi na kuchukuliwa na wenyewe, wakifungua wanakwenda kuziuza kwenye maduka ya āspareā Kariakoo au katikati ya jiji.
āWanunuzi wengine ni wenye magereji yanayotengeneza magari makubwa na wana wateja wao pia ambao ni wamiliki wa magari makubwa ambayo yanakuwa yanahitaji āspareā baada ya zilizopo kuchoko, wakishawauzia huwa wanapitia gerezani na kununuaĀ Ā āspareā zilizochoka na kuja kuzifunga pale walipotoa mpya.
āNdiyo maana waagizaji magari kila mara wanalia magari wanayoagiza kuwa yanakuja na vipuli vilivyochoka na au wanayakuta magari yao hayana baadhi ya vipuli, chanzo cha yote haya ni wizi unaofanyika kwenye hii yadi na Issac anajua kila kitu.
āNa tunashangaa kwa sababu yadi hii kama zilivyo nyingine kazi yake ni kuhifadhi magari ambayo hayajalipiwa kodi lakini hii sasa pamoja na kutumika kama yadi inatumika pia kama karakana, sijui sheria inasemaje katika hili,ā kilisema chanzo chetu cha habari.
Alipoulizwa Issac Abdallah ambaye ofisi yake ipo kwenye kona ya Barabara ya Lumumba na Mtaa wa Amani katika Jengo la Rissa Barbaque,Ā ghorofa ya tano, kuhusu tuhuma hizo alikiri yadi yake kujishughulisha na shughuli za utengenezaji magari mbali ya kuyahifadhi kama ulivyo utaratibu wa kawaida kwa kile alichoeleza kuwa ingawa ana leseni ya kuhifadhi magari lakini ameruhusiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kufanya shughuli za utengezaji magari ndani ya yadi hiyo.
Rekodi zilizopo zinaonyesha kuwa awali, Issac ambaye pia hujishughulisha na biashara ya kuuza magari alikuwa na yadi ya magari huko Sinza, Dar es Salaam akiwa na ushirika wa kibiashara na raia mmoja wa Pakistani ambaye alipata kukamatwa kwa makosa ya kukwepa kulipa kodi kabla ya kudhaminiwa na kutimka kutoka hapa nchini.
Tanzania PANORAMA Blog inaendelea na uchunguzi wa suala hili. Ā Ā Ā Ā Ā Ā
Ā