Monday, December 23, 2024
spot_img

TAZA KUUNGANISHA UMEME AFRIKA

TERESIA MHAGAMA

MRADI wa ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 400 wa TAZA, kutoka Iringa hadi Sumbawanga mkoani Rukwa unaweza kutandazwa Afrika nzima hivyo kuliunganisha bara hilo kwa nishati ya umeme.

Kwa hatua ya ujenzi wa sasa, TAZA itaunganisha Tanzania na Zambia pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tagamenda, Kisada, Iganjo, Nkengamo na Malangali na unaweza kutanuliwa ukaanzia Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa mwezi uliopita na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo huko Sumbawanga mkoani Rukwa.

Alisema mradi huo ni mkubwa ukihusisha kipande cha kilomita 4 kutoka Mji wa Tunduma Tanzania hadi Mji wa Nakonde Zambia.

“Kwa kutambua kuwa nishati ni kichocheo cha uchumi, Serikali inaendelea kutekekeza miradi mbalimbali ukiwemo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambao tayari unaingiza megawati 705 kwenye gridi ya Taifa.

“Hatua hizi zitaiwezesha nchi kuwa na ziada ya umeme na mtambo mwingine wa
megawati 235 unatarajiwa kuwashwa mwezi Agosti mwaka huu,” alisema.

Aliitaja miradi mingine inayotekelezwa na Serikali kuwa ni wa umeme Jua wa Kishapu (MW 150), Malagarasi (MW 49.5) na ya gesi asilia.


Dk. Biteko alisema uzalishaji wa umeme lazima uendane na kazi ya uungashiaji umeme kwa wananchi kupitia miradi mbalimbali ukiwemo wa TAZA.

Alisema Mkoa wa Rukwa unapata umeme kutoka nchini Zambia kwa gharama ya Shilingi 15 bilioni kwa mwaka hivyo kukamilika kwa mradi wa TAZA kutaifanya Tanzania kuacha kununua umeme kutoka Zambia isipokuwa nyakati za dharura.

Dk. Biteko alisema TAZA utafaidisha pia maeneo yanayopitiwa na mkuza kutoka mkoani Iringa hadi Rukwa, kupitia vituo vya kupoza na kusambaza umeme hivyo Tanzania itaweza kuuza umeme katika nchi za Mashariki ya Afrika kupitia ‘Southern African Power Pool (SAPP) na Easten Africa Power Pool (EAPP).’

Alilipongeza Shirika la Ugavi wa Umeme  (TANESCO) kwa utendaji kazi mzuri na aliliagiza kusimamia kasi ya utekelezaji mradi wa TAZA.

Wakati huo huo, Dk. Biteko alisema hafurahishwi na kazi ya usambazaji umeme vijijini katika Mkoa wa Rukwa inayofanywa na mkandarasi na kuwagiza Katibu wa Wizara ya Nishati na Mkurugenzi wa REA kuchukua hatua za kimkataba kwa mkandarasi ifikapo Agosti mwaka huu iwapo atakuwa hajakamilisha kazi.


“Kazi za kusambaza umeme vijijini zinaombwa na kampuni za nje ya nchi na kampuni za ndani. Tunaonekana wabaya kwa kuzibana sana kampuni za nje lakini za ndani tunabembelezana, Katibu Mkuu na DG REA nataka nione hatua zinachukuliwa.

“Haiwezekani wakandarasi wageni tunawabana halafu wa ndani wanaharibu miradi, wananchi wanalalamika lakini tunabembelezana, hii Hapana,” alionya Dk. Biteko.

Alisisitiza kuwa Serikali inakusudia kukamilisha kazi ya usambazaji umeme vijijini ili ianze kwenye vitongoji, lengo likiwa kufikisha umeme kwenye vijiji  vyote ifikapo Disemba, mwaka huu.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya