ANDREW CHALE
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (MNEC – CCM) Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas anatarajiwa kufanya ziara maalum katika mkoa huo ambapo pia atakutana na Halmashauri Kuu za CCM Wilaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Iringa ziara hiyo inatarajia kuanzia Mufindi siku ya Jumamosi Agosti 3, mwaka huu.
“Tarehe 3 Agosti, 2024 Mufindi, Tarehe 4 Agosti, Kilolo, Tarehe 7 Agosti, Iringa Vijijini na mwisho atahitimisha tarehe 9 Agosti, Iringa mjini,” inasomeka taarifa hiyo.
Asas ameendelea kukiimarisha CCM katika Mkoa wa Iringa huku akiwa nguzo kwenye kushiriki miradi ya kimaendeleo kimkoa, Nyanda za Juu Kusini pamoja na Taifa kwa ujumla.
Pia anasifika kwa utendajikazi, ustamilivu, subra, busara, huruma na mapenzi yake kwa CCM na Taifa vimeendelea kumjengea taswira njema kwa wananchi.
Aidha, amekuwa mstari wa mbele kujitolea katika Sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, mitaji ya wafanyabiashara wadogo (machinga), vijana na kinamama, lishe mashuleni, michezo na mengine mengi.