Monday, December 23, 2024
spot_img

KIGWANGALLA ABEZA BIL. 6 ZA USAJILI SIMBA

RIPOTA PANORAMA

MBUNGE wa Nzega vijijini na shabiki mkubwa wa timu ya Simba amebeza usajili wa matumizi makubwa ya fedha za mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji kuwa ni ya kupaka rangi ufa.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa X, zamani twitter hivi karibuni, Kigwangalla anaeleza kuwa ameona bajeti ya mwekezaji kwenye usajili wa msimu huu ya Sh. bilioni 6 na ameona masimango mengi dhidi yake kutoka kwa aliowaita mbumbumbu.

Katika andiko lake hilo, Kingwangalla anaeleza kuwa hatachoka kutoa elimu ya bure bila kujali kama inatakiwa au haitakiwa kwa sababu hakuna elimu mbaya na hakuna ukweli ulioaibika.

“Ni suala la muda tu kabla haujasimama na kuthibitika. Ukweli huwa una mwendo wa kinyonga, uongo una mabawa kama tai. Kama hatujarekebisha mfumo na muundo wa timu yetu hata mwekezaji aweke nini hakutakuwa na mafanikio ya kutisha.

“Kuna siku mtanikumbuka. Iko hivi, hakuna alichonacho tajiri mwenye elimu akakosa, kilichofanyika ni kupaka rangi ufa  na siyo kurekebisha ukuta,” unasomeka ujumbe wa Kigwangalla.

Mohammed Dewji

Anaandika pia kuwajibu aliowaita mbumbumbu wanaomdhihaki wakimtaka asajili walau mchezaji mmoja akieleza kuwa hashindwi kusajili kwani msuli huo anao na kwamba yeye siyo masikini kwani hapo awali alichangia sana mafanikio ya timu ya Simba bila kujitangaza kwa sababu hakuwa anatafuta chochote.

“Lakini kwa wenye mantiki watahoji kwamba nisajili kama nani? Ili iweje? Mfumo mpya umefeli? Najiuliza, najiliuza mwekezaji kaweka bilioni 6 lini? Mchanganuo wake upo wapi? kaziweka kama kitu gani?

“Najiuliza najiuliza mapato ya mwaka jana ni yepi? Anatangaza bidhaa zake kwa minaajili ipi? Yeye mwenyekiti wa bodi kwa miajili ipi? Hisa kalipa ama lah? Jibu hajalipia, anatoa wapi mamlaka na madaraka ya kuteua bodi hajalipia hisa zake? ni kwanini mbumbumbu mnafurahi? Ama kweli ni mbumbumbu?” anahoji Kigwangalla kwenye ujumbe wake.

Anahitimisaha ujumbe wake kwa kuhoji zaidi kuwa ni nini kimekwamisha mabadiliko ndani ya klabu ya Simba kwa kipindi cha miaka saba sasa na matangazo ya mwekezaji yanaiingizia kiasi gani klabu ya Simba na kinatumikaje.

Ujumbe huo wa Kigwangalla ambao umechangiwa na wengi kwa mitizamo tofauti umewaibua baadhi ya watu wanaodai kuwa sasa umefika muda kwa Dewji kutumia misuli yake kuanika kilichojificha nyuma ya ukoasaji wenye mwelekeo wa mashambulizi binafsi dhidi ya mwekezaji huyo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya