Tuesday, December 24, 2024
spot_img

TBS YAIBUA UTATA MAGARI YANAYOUNDWA KWA SPEA CHAKAVU NA METL 

CHARLES MULLINDA

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeibua utata kuhusu ukaguzi wa magari yanayoundwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited (METL) kwa kutumia spea chakavu.

TBS imesema magari yanayoundwa na METL kwa kutumia spea chakavu siyo shughuli iliyosajiliwa na ukaguzi wake haufanyiki mara kwa mara.

Afisa Masoko wa TBS, Deborah Haule ndiye aliyeeleza hayo alipokuwa akijibu maswali ya Tanzania PANORAMA Blog kuhusu aina ya magari yanayoundwa na METL kwa kutumia spea chakavu yanayokaguliwa na kupasishwa na shirika hilo.

Haule ametaja magari hayo kuwa ni malori tofauti na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa METL, Gullam Dewji kupitia kwa msaidizi wake aliyejitambulisha kwa jina moja la Rachel kuwa kampuni hiyo ina vibali vya serikali vya kuunda magari hapa nchini kwa kutumia spea chakavu inazoagiza kutoka nje ya nchi.

“Zoezi la ukaguzi wa magari aina ya rebuilt trailers yanayoundwa na kampuni tajwa kwa kutumia spea zilizotumika sio wa mara kwa mara na sio shughuli iliyosajiliwa ili kuweza kupata muda kamili.

“Utaratibu iliopewa kampuni tajwa ni kuomba ukaguzi wa kila rebuilt road trailer iliyoundwa kwa kutumia spea zilizotumika pindi linapokamilika ili kufanya ukaguzi kwa kutumia utaratibu wa ukaguzi kwa magari yaliyotumika (used motor vehicles), na kampuni tajwa imekuwa ikifanya hivyo.

Wakati TBS ikieleza hayo, Gullam Dewji yeye amekwishaeleza kuwa kampuni yake ya METL ina vibali vya serikali vya kuunda magari hapa nchini kwa kutumia spea chakavu inazoagiza kutoka nje ya nchi.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Yusuph Mwenda

Dewji alisema biashara yake ya kuunda magari kwa kutumia spea chakavu imesajiliwa na uagizaji wa spea chakavu kutoka nje ya nchi unazingatia ulipaji ushuru wa serikali.

Alisema kodi zote stahiki zinalipwa na magari yanayoundwa kwa spea hizo chakavu yanakaguliwa na Shirika la Viwango (TBS) kabla ya kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Tanzania PANORAMA Blog ilimuuliza Dewji ni lini METL ilipata kibali cha kuunda magari kwa kutumia spea chakavu, na tangu kuanza mpaka sasa ni magari mangapi ambayo kampuni hiyo imeunda kwa kutumia spea chakavu, mangapi yanatumika na iwapo magari hayo ni kwa ajili ya METL pekee au huingizwa sokoni kuuzwa kwa wateja wengine.

Dewji alijibu kupitia kwa Rachel akieleza kuwa biashara ya magari, kama zilivyo biashara zake nyingine, inafuata sheria na kanuni zote za nchi na kwamba hawezi kuzungumzia kiundani biashara zake bali wanaoweza kufanya hivyo ni TBS, Mamlaka ya Mapato (TRA) na BRELA. 

Taarifa zilizopo na uchunguzi uliofanywa na Tanzania PANORAMA Blog, vinaonyesha wapo watu na kampuni binafsi zinazonunua magari mapya nje ya nchi kisha kuyakatakata au kuyaachanisha na kuyasafirisha kwenye kontena kama spea chakavu hadi hapa nchini.

Vipande hivyo vya magari ambavyo huingizwa nchini kama spea chakavu huunganishwa na kuwa magari ambayo huingia barabarani kutumika yakiwa hayajalipiwa kodi stahiki. Inadaiwa zaidi kuwa ujanja huo unatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi.

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hasaan amekuwa akisisitiza uzibaji wa mianya ya ukwepaji kodi na hivi karibuni alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, akiwamo Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alisema amemteua kijana, mtoto wa mjini ambaye uhuni wa TRA umefanywa yeye akiwa humo hivyo akageuza sura yake.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi na Huduma kwa Wateja wa TRA, Hudson Kamoga alilizungumzia hilo kwa kueleza kuwa kazi ya TRA siyo kusajili biashara bali kutoza kodi.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi na Huduma kwa Umma wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Hudson kamoga

Kamoga alielekeza mzigo kwa taasisi za ukaguzi ubora kwa kusema mfumo wa ulipaji kodi una mnyororo mrefu unaohusisha taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo za udhibiti ubora na ukaguzi wa bidhaa ambazo baada ya kukamilisha kazi zake ndipo TRA hutoza kodi husika kwa kuzingatia nyaraka zilizoidhinishwa na taasisi hizo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya