Monday, December 23, 2024
spot_img

TABASAMU, MAKUNYANZI KUNG’OLEWA KIDATA TRA

RIPOTA PANORAMA

ALPHAYO Japan Kidata, (pichani hapo juu) ameng’olewa kwenye nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), amepelekwa Ikulu kwenda kuwa Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais, Ikulu.

Kung’olewa kwa Kidata katika mabadiliko ya viongozi yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na kutangazwa jana usiku, kumeacha picha mbili tofauti zinazoonekana kwenye uchunguzi wa kiuanahabari uliofanywa na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu mgogoro uliopo kati ya TRA na wafanyabiashara.

Picha zinazoonekana kwenye uchunguzi wa Tanzania PANORAMA Blog ambao uko mbioni kuchapishwa, ni za makundi mawili tofauti yaliyopo katika sakata la TRA na wafanyabiashara; kundi la kwanza likiwa la wafanyabiashra waliokuwa wakipambana kulipa kodi kidogo kwa mizigo wanayoingiza kutoka nje ya nchi; kundi ambalo sasa litakuwa linatabasamu.

Kundi la pili ni la watendaji ndani ya TRA waliokuwa wakitekeleza majukumu yao bila woga huku wakisaka kodi stahiki ya serikali kwa kila mfanyabiashara anayepaswa kulipa na pamoja nao ni wananchi waliokuwa wakifurahia utendaji wa TRA wa kubana mianya ya ukwepaji kodi na pia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi. Kundi hili litakuwa na makunyazi usoni.

Taarifa zilizokusanywa kwenye uchunguzi zinaonyesha kuwapo kwa mnyukano mkali baina ya TRA na wafanyabiashara wenye ukwasi mkubwa, ambao sasa wanaitwa TRA ndogo wanaonufaika na fedha za wafanyabiashara wenye mitaji midogo na ile ya kati wanaowangizia mizigo na kuilipia kodi wao.

Uchunguzi unaonyesha kuwa wapo wafanyabiashara wachache wakubwa ambao wamekuwa wakisajili wafanyabiashara wengi wenye mitaji midogo na ya kati kuwaagizia bidhaa nje ya nchi ambao huwataka kulipa kwao fedha za kodi za mizigo yao ili wao walipie kodi ya jumla ya mizigo yote inapoingia.

Imebainika baada ya shehena ya mizigo kufika nchini hulipiwa kodi ya jumla na wafanyabiashara hao wakubwa na wakiwa tayari wamekwishaweka kibindoni fedha walizokusanya kwa wafanyabiashawa wadogo na wa kati waliowaingizia mizigo huwapatia bila risiti kwa sababu risiti ya mizigo yote inakuwa moja kama ilivyolipwa kwa TRA.

Wafanyabiasha wanaoagiziwa bidhaa na TRA ndogo licha ya kupata nafuu kubwa ya kulipa kodi na kupelekewa mizigo yao kwenye maghala yao bila kupewa risiti za kodi huwa wanajikuta kwenye wakati mgumu wanapofikiwa na maafisa wa TRA wanaokagua risiti za kodi.

Uchunguzi umebaini kuwa hatua hiyo ya TRA kusaka kodi kwa wafanyabiashara wanaoingiziwa mizigo kutoka nje ya nchi na TRA ndogo au wafanyabishara wakubwa, ni moja ya sababu za mgogoro wa hivi karibuni baina ya TRA na wafanyabiashara hata kufikia hatua ya baadhi yao kupaza sauti za kutaka Kidata aondolewe TRA.

Yusuph Juma Mwenda ambaye anarithi mikoba ya Kidata, anaingia ofisini akikabiliwa na mtihani mkubwa wa kupambana na TRA ndogo na haina shaka iwapo atachukua mwelekeo wa Kidata atakabiriwa na upinzani ule ule aliokabiliana nao Kidata.

Tanzania PANORAMA Blog itachapisha ripoti maalumu kuhusu kilichojificha nyuma ya mgogoro uliozaa mgomo wa wafanyabiashara nchini.       

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya