Monday, December 23, 2024
spot_img

UPO WAPI MKURABITA 2004/2024?

BUBERWA KAIZA

WATANZANIA na viongozi wetu kuna jambo lolote tulilojifunza kuhusu nafasi ya raia wenyewe kubuni na kuasisi sera na mipango yao ya maendeleo? Uko wapi MKURABITA 2004/2024?

Serikali ya Hayati Benjamin Mkapa iliamini kupita kiasi mawazo ya maendeleo ya kigeni hadi ikamleta Profesa Hernando de Soto, mchumi kutoka nchini Peru aliyekuwa kiongozi wa Shirika Lisilokuwa na Kiserikali (NGO) lililofahamika kwa jina la The Institute for Liberty and Democracy (ILD) kuja kuisaidia serikali na watanzania kufikiria namna ya kubuni sera za kumaliza umaskini miongoni mwa watanzania na Tanzania.

Mwaka 2003 Profesa de Soto, akiwa mgeni rasmi wa Serikali na Rais Mkapa mwenyewe, alikuja na ILD yake hapa nchini na kupewa heshima kubwa. 

Si serikali wala Rais Mkapa aliyekuwa tayari kusikia mawazo ya maprofesa wa hapa nchini, miongoni mwao Gulam Hussein Issa Shivji, Samuel Wangwe, Mwesiga Baregu, Teddy Maliyamkono na Anna Tibaijuka.

Watawala hawakutaka hata kurejea maarifa ambayo marehemu Profesa Justini Rweyemamu aliyatoa miaka 20 nyuma au yale ya Profesa Mboya Bagachwa aliyoyatoa miaka mitatu kabla ya ujio wa De Soto.

Profesa Anna Tibaijuka

Mawazo ya wasomi wetu hao kuhusu namna bora kwa Afrika, hususan Tanzania kuondokana na umaskini, yaliachwa kwenye maandishi.

Serikali ikiongozwa na mawazo ya Profesa De Soto, mwaka 2004 ilianzisha Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Leo ni miaka 21, MKURABITA umebaki kuwa ndovu mweupe, mafanikio yake makubwa yakiwa kuendesha semina na warsha kuhusu umaskini ambao hata hivyo, kimsingi, unaongezeka.

Haidhuru maofisa wa serikali wanapata posho na kutunisha mifuko yao kutoka kwenye kupanga au kuhudhuria semina na warsha za MKURABITA lakini kwa walengwa wanachoongeza hakipo.

Profesa Issa Shivji

Kitendo pekee cha maendeleo kinachoonekana ni kuhamisha Ofisi ya MKURABITA kutoka Sea View Jijini Dar es Salaam kwenda Dodoma.

MKURABITA au sera nyingine yoyote ile ya kuondoa umasikini ingebuniwa na wataalamu wetu, leo Watanzania tungekuwa na fursa ya kuwawajibisha lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa Profesa Hernando de Soto anayeendelea kuuza ILD yake kwenye anga za kimataifa.

Ni wakati sasa wa kuwaamini na kuwawajibisha wanazuoni wetu katika masuala yetu yote ya kisera.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

1 COMMENT

  1. Asante kwa kutuhabarisha masuala nyeti kitaifa. Hili la vita vipya vya bima vya Afya ni hatarishi. Wananchi waelememishwe na kusimama kidete kupings

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya