TERESIA MHAGAMA
WIZARA ya Nishati na taasisi zilizo chini yake imeshiriki maadhimisho ya wiki ya utumishi yaliyoanza Juni 16 Juni 2024 katika viwanja vya Chinangali, Jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yanayofikia tamati Juni 23, 2024 yanahudhuriwa na wataalamu wa Wizara ya Nishati na taasisi zake ambao wanatoa huduma kwa wananchi wanaohitaji huduma zinazotolewa katika Sekta ya Nishati.
Sambamba na kutoa huduma kwa wananchi, watalaamu wa wizara hiyo pia wanatoa elimu kuhusu utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa Nishati Safi ya kupikia, utekelezaji wa miradi ya umeme, mafuta na gesi asilia.
Aidha, katika Banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)Â yanafanyika maonesho ya shughuli za uchimbaji wa gesi asilia, usafirishaji na uchakataji wake kupitia teknolojia ya uhalisia pepe ( Virtual Reality) na maelezo kuhusu juhudi za serikali za uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia.
Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), yanafanyika maonesho ya utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere ( JNHPP) kupitia kifaa cha uhalisia pepe na ambapo wateja wanapata huduma ya kuunganishwa umeme kupitia mfumo wa simu janja wa Nikonekt na wanaelimishwa kuhusu nishati safi ya kupikia kwa majiko yanayotunza umeme, kushughulikiwa changamoto za mita mabadiliko ya mita za LUKU.
Katika Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatolewa huduma ya moja kwa moja ya nishati safi ya kupikia kupitia wadau wa usambazaji na waendelezaji wa teknolojia husika, elimu ya usambazaji umeme vijijini na vitongojini na uendelezaji wa miradi midogo ya umeme.
Taasisi nyingine za Wizara ya Nishati zinazoshiriki maadhimisho hayo ni mamlaka ya udhibiti wa mkondo wa juu wa Petroli ( PURA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambao wanatoa elimu kwa umma kuhusu shughuli za udhibiti.
Aidha, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) inashiriki maonesho hayo kwa kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za nishati na maji, ikiwa ni taasisi inayosimama kama sauti ya watumiaji wa huduma husika
Maadhimisho ya mwaka 2024 yamebebwa na kauli mbiu isemayo ‘kuwezesha utumishi wa umma uliojikita kwa umma wa Afrika ya Karne ya 21 uliyojumuishi na inayostawi; Ni safari ya mafunzo na mabadiliko ya kiteknolojia.’
Ninaomba kufanya kazi nanyi