Friday, July 18, 2025
spot_img

DIALLO AJIWEKA KANDO SKANDALI YA MBOLEA YA BIL. 7.9

RIPOTA PANORAMA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA), Anthony Diallo amejiweka kando na skandali inayoiandama Kampuni ya Mbolea (TFC) ya kusigina sheria za manunuzi ya umma na ubatili wa nyaraka za fedha katika manunuzi, usambazaji na uuzaji wa tani 4500 za mbolea yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 7.9.

Amesema anayepaswa kujibu hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi wa Ndani wa TFC kuhusu manunuzi, usambazaji na uuzaji wa mbolea hiyo ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Samuel Ahad Mshote.

Akizungumza jana na Tanzania PANORAMA Blog kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu skandali hiyo, Diallo alisema yeye kama Mwenyekiti wa Bodi wa TFRA ana utaratibu wake wa kuzungumza na kusisitiza kuwa Mtendaji Mkuu wa TFC ndiye anayepaswa kutoa majibu ya hoja zilizoibuliwa na mkaguzi wa ndani.

“Hayo muulize mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ndiye anayepaswa kutoa majibu, mimi nina utaratibu wangu mwingine wa kuzungumza kama mwenyekiti wa bodi lakini kwa hayo unayoniuliza, majibu yake anapaswa kuyatoa mtendaji mkuu,” alisema Diallo.

Wakati Diallo akitoa kauli hiyo, Tanzania PANORAMA Blog inazo taarifa kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya TFRA, katika kikao chake cha hivi karibuni, pamoja na mambo mengine ilijadili kwa kina ripoti ya Mkaguzi wa Ndani wa TFC iliyoibua ‘madudu’ kwenye manunuzi ya mbolea hiyo.

Haikufahamika mara moja uamuzi uliofikiwa kwenye kikao hicho cha bodi ya wakurugenzi ingawa zipo taarifa zilizodai kuwa mzigo wote wa skandali hiyo alitwishwa Mkurugenzi Mkuu Mshote.

Katika ripoti yake Mkaguzi wa Ndani wa TFC anaeleza kubaini manunuzi, usambazaji na uuzaji wa tani 4500 za mbolea yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 7.9 yalifanyika bila ya kutangaza tenda.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea, Samuel Ahad Mshote.

Mkaguzi huyo anaeleza katika ripoti yake kuwa TFC haina nyaraka yoyote iliyoandaliwa na menejimenti kwa ajili ya manunuzi hayo, hakuna kikao chochote kilichoketi kuamua kufanyika kwa manunuzi na kwamba bodi ya zabuni ya kampuni haikushirikishwa.

Anaeleza zaidi kuwa katika ukaguzi wake alibaini kuwepo kwa tofauti ya takwimu za mauzo kati ya kumbukumbu zilizowekwa na TFRA na rekodi zinazowekwa na TFC na kwamba rasimu ya taarifa za fedha iliyowasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Agosti, 2023 ya mauzo ya mifuko 77,827 ya mbolea ina walakini.

Aidha, ripoti hiyo inaonyesha kuwa idara yenye dhamana ya kuweka salio la hisa za mbolea nayo haina kumbukumbu sahihi za hisa za mbolea kutoka kwenye maeneo  ya mauzo.

Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Samuel Ahad Mshote ambaye amekuwa akiulizwa kila mara kuhusu skandali hiyo, amekaa kimya.

    

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya