Thursday, July 17, 2025
spot_img

PAPA: NDOA IAKISI MUUNGANIKO WA MWANAUME NA MWANAMKE

VATICAN

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisco amewataka waumini wa kanisa hilo duniani kutekeleza utimilifu wa ndoa kati ya mwanamke na mwanaume.

Ujumbe huo wa Papa Francisco umo kwenye wosia wake wa kitume alioutoa wakati wa sikukuu ya Krismas ambao kwa lugha ya kiratini unafahamika kama Aamoris Laetitia.

Kwa mujibu wa tovuti ya Vatican, ujumbe huo ambao maana yake halisi ni furaha na upendo ndani ya ndoa, umezingatiwa pia katika mafundisho tanzu ya kanisa, ambayo kwa lugha ya kilatini yanafahamika kama Fiducia supplicans, yaliyotolewa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Disemba 18, 2023.

Katika wosia wake huo, Papa Francisco aliwataka wakristo ulimwengu kote kuifanya ndoa ya kikristo kuakisi muunganiko kati ya Yesu Kristu na Kanisa Katoliki.

Ameeleza kuwa mwanaume na mwanamke wanaojitoa kila mmoja kwa mwenzie kwa upendo ulio huru, uaminifu na kila mmoja kuwa mali ya mwenzake hadi kufa wakiendeleza kizazi chao, wanakuwa na wakfu kwa sakramenti inayowaletea neema ya kuwa kanisa la nyumbani na chachu ya maisha mapya kwa jamii.

Papa aliwaasa waumini wa kanisa hilo kuwa upendo unapaswa kuoneshwa kwa kujikita katika uelewa, uvumilivu, huruma na ujasiri bila kuwahukumu wengine kuwa ni wadhambi!

Papa Francisco akisalimiana na familia ya kikatoliki.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Kardinali Kevin Joseph Farrell, katika ujumbe wake kwa siku ya familia takatifu ya Yesu, Maria na Yosef alisema maisha ya ndoa na familia yanajenga na kudumisha uhusiano na ufungamano ili ndoa ziwe kanisa dogo la nyumbani.

“Huu ni wakati wa wanafamilia kukaa pamoja, kukazia malezi bora na utu wema. Ni wakati wa kujenga na kudumisha utamaduni wa majadiliano katika ukweli na uwazi kwa kusikilizana, kuheshimiana na kuthaminiana.

“Ni muda wa kuratibu vema rasilimali muda kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya familia.

“Ni muda wa wanandoa kuangaliana usoni bila kupepesa pepesa macho ili kujenga na kuimarisha upendo na urafiki wao wa dhati, daima wakimwachia nafasi Kristo Yesu,” alisema Kardinali Ferelli.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya