Monday, December 23, 2024
spot_img

VATICAN YATAKA MAZUNGUMZO HARAKA VITA YA ISRAEL, HAMAS

VATICAN

KATIBU wa Vatican wa Mambo ya Nje na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu, Paul Richard Gallagher, amesema yanahitajika mazungumzo ya haraka kutatua mzozo baina ya Israel na Kikundi cha Kigaidi cha Hamas.

Akizungumza Disemba 23, 2023 katika mahojiano maalamu ya Gazeti la Jimbo la Rome la Satte, linalochapishwa kila wiki, Askofu Mkuu Gallagher alizungumzia vita ya Israel na Kundi la Kigaidi la Hamas, vita ya Ukreini na Urusi na msuguano baridi wa Umoja wa Mataifa (UN) na China.

Alisema Oktoba 7, 2023 dunia ilishuhudia ukatili wa kutisha ambao hauna uhalali wowote lakini pia kilichotokea baada ya ukatili huo hakikubaliki hivyo kuna haja ya kuwepo mazungumzo ya haraka kukomesha hali hiyo.

Askofu Mkuu Gallagher alisema anayo matumaini vita ya Israel na Kundi la Kigaidi la Hamas haitaibua migogoro mingine ya kidini na haitarefushwa kwa sababu maisha ya mwanadamu ni ya muhimu.

Akizungumzia vita vinavyoendelea kwa takribani miaka miwili sasa, baina ya Urusi na Ukreini, Askofu Mkuu Gallagher alisema kuendelea kwa vita hiyo kuna sababisha maafa kwa watu wasiokuwa na hatia  

“Kukwama kumalizika kwa vita hiyo kunasababisha maafa kwa pande zote mbili zinazopigana. Tunaendelea kusisitiza upatanishi. Tunachoweza kufanya sasa ni kutoa misaada ya kibinadamu.

“Tunaendelea kutumia ofisi zetu nzuri kwa ajili ya kubadilishana wafungwa na kujaribu kuwezesha mpango wa kuwarejesha makwao watoto wa Ukreini. Ni lazima tukubali kwamba matokeo ya jitihada hizi ni ya kawaida hata kama ni magumu. Lakini tunaendelea kufanya kazi,” alisema. 

Aidha, Askofu Mkuu Gallagher alisema Papa Francisko anayo nia ya kufanya ziara katika mataifa ya Urusi na Ukreini ambayo lengo lake ni kusaidia kutuliza uhasama uliopo baina ya mataifa hayo.

Askofu Mkuu Paul Galagher

 “Papa bado yuko wazi sana kwenda Ukreini na Urusi, itakuwa ishara ya kutuliza uhasama uliopo baina ya mataifa hayo lakini kwa bahati mbaya hatufikirii itakuwa lini.

“Tunatumaini itakuwa hivi karibuni lakini pia inategemea mwitikio wa nia ya Papa kwa pande zinazozozana. Ninatamani kwamba ziara ya Papa ingethaminiwa na pande zote mbili zinazozona,” alisema Askofu Mkuu Gallagher.

Kuhusu Mashirika ya Umoja wa Mataifa, alisema mengi yanafanya kazi nzuri na yanatoa mchango muhimu katika maeneo ya vita lakini kwenye nyanja za kisiasa na kidiplomasia yanakabiliwa na changamoto zinazozoretesha kazi zake.

Alisema upo umuhimu wa kuimarisha majukumu ya Balaza la Usalama wa Umoja wa Mataifa na kuongeza wajumbe wasiokuwa wa kudumu ndani ya baraza hilo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya