Tuesday, December 24, 2024
spot_img

MWANAHARAKATI NA MKOSOAJI WA SERIKALI YA RWANDA AFARIKI DUNIA MAREKANI

MASHIRIKA YA HABARI

MWANAHARAKATI na mkosoaji wa Serikali ya Rwanda, Anne Uwamahoro Rwigala (41), amefariki duniani akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Utangazaji wa Uingereza (BBC), Rwigala ambaye alikuwa na uraia wa Marekani, alikutwa na umauti huko California, Marekani.

BBC limemkariri mama yake Rwigala, Adeline Rwigala kuwa mwanaye hakuwa mgonjwa na kwamba kifo chake ni fumbo.

Mwanaharakati Anne Uwamahoro Rwigara, mtoto wa aliyekuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa ya kibiashara nchini Rwanda, Marehemu Assinapol Rwigara alipata kufungwa gerezani kwa siku kadhaa nchini humo kwa tuhuma mbalimbali.

Marehemu Anne Rwigala alifungwa pamoja na mama na dada yake, Diane Rwigala baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017; uchaguzi mkuu ambao dada yake aliyekuwa ameonyesha nia ya kuchuana na Rais Paul Kagame, alizuiwa kugombea.

Katika uchaguzi huo, Rais Kagane alipata ushindi wa takriban asilimia 99 ya kura zote  zilizopigwa.

BBC limeripoti kuwa hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu sababu ya kifo chake.

Kifo cha ghafla cha Anne Rwigala kimeibua kumbukumbu ya kifo cha baba yake, Marehemu Assinapol Rwigara kilichotokea mwaka 2015 kwa kile ambacho polisi walieleza kuwa alifariki kwa ajali ya barabarani.

Familia ya Marehemu Rwigala alidai kuwa aliuawa katika ajali iliyopangwa na ilimwandikia barua Rais Kagame ikimtaka achunguze kifo chake.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya