Monday, December 23, 2024
spot_img

UAMUZI WA KUMSIMAMISHA WAKILI MPOKI WALAANIWA

RIPOTA PANORAMA

UAMUZI wa Kamati ya Maadili ya Mawakili, kumsimamisha Wakili Mpale Kaba Mpoki kufanya kazi za uwakili kwa muda wa miezi sita umelaaniwa.

Taarifa ya kulaani uamuzi huo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Utetezi Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Paul Kisabo kwa niaba ya mashirika matatu yenye wanasheria gwiji wa masuala ya kisheria.

Mashirika hayo ni Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Muungano wa Wanasheria wa Pan African (PALU).

Taarifa hiyo inalaani na kueleza wasiwasi wa wanasheria hao kuwa uamuzi wa kumsimamisha Wakili Mpoki unatia shaka mchakato unaostahili haki na haki ya kutafuta suluhu ya kisheria.

Inaeleza kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili alitoa uamuzi wa kumsimisha Wakili Mpoki wakati Kamati ya Maadili ya Mawakili ilipokuwa ikisikiliza shtaka la kimaadili linalomkakabili Wakili Boniface Mwambukusi. Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili inayosikiliza shtaka la kimaadili linalomkabili Wakili Mwambukusi ni Jaji Ntemi Kilekamajenga

Wakili Mpoki aliyekuwa miongoni mwa mawakili waliokuwa wakimtetea Wakili Mwakumbukusi katika shtaka linalomkabili, ‘alitiwa kitanzi’ cha miezi sita kutofanya kazi ya uwakili alipokuwa akitoa hoja za utetezi.

Wakili Mpale Mpoki

Kwa mujibu wa taarifa, Wakili Mpoki aliibua hoja kadhaa za pingamizi la awali dhidi ya mamlaka ya kamati ambazo baada ya kusikilizwa na kamati, hoja tatu kati ya alizotoa na zilipitishwa.

Inaeleza zaidi kuwa, Wakili Mpoki baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa mteja wake, Wakili Mwambukusi alieleza nia ya mteja wake huyo kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa kamati hiyo lakini Jaji Ntale alitoa uamuzi wa kumsimamisha kufanya kazi ya uwakili kwa muda wa miezi sita.  

Taarifa inaeleza zaidi kuwa uamuzi wa kumsimamisha kazi wakili aliyetoa hoja ya mteja wake kukata rufaa unadhoofisha uadilifu wa taaluma ya sheria, unyanyasaji na ukiukaji haki ya kufanya kazi kwa wakili huyo.

Inatoa rai kwa kamati ya mawakili kuangaliwa upya uamuzi huo na kuheshimu kazi za mawakili na pia inahimiza kuzingatia kanuni za haki, mchakato unaostahili na haki za mawakili ili kudumisha uadilifu wa mfumo wa sheria.


Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya