Tuesday, December 24, 2024
spot_img

BITEKO AZINDUA MITAMBO YA UMEME KIJIJI CHA IHAKO

TERESIA MHAGAMA NA GODFREY LULINGA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amezindua mitambo ya kusambaza umeme katika Kijiji cha Ihaka, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.

Biteko alizindua mitambo hiyo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Bukombe ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ihako baada ya kuzindua mitambi huyo, Biteko alipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi ya kusambaza umeme vijijini.

Alisema kuwashwa umeme katika Kijiji cha Ihako ni mwendelezo wa mchakamchaka wa kupeleka umeme kwa wananchi wote waliopo vijijini.

“REA nendeni vijijini, muda wa kufanya vikao kwenye kumbi kubwa kubwa
au makao makuu ya miji hatutaki, tunataka tuwaone mnaenda vijijini kupeleka umeme.

“Nyie ni Wakala wa Nishati Vijijini siyo Wakala wa Umeme Mijini, vikao vyenu viwe na wananchi na magari yenu yapite humo wanamopita wananchi wenye maisha ya kawaida kabisa,” alisisitiza Biteko.

Alisema Serikali inataka kuona kazi ya kusambaza umeme vijijini inafanyika na uingie kwenye nyumba zote bila kubagua kwa sababu kila mwananchi anahitaji umeme.

Aidha, alitaka maeneo yenye changamoto za umeme utatuzi wake upewe kipaumbele badala ya kumsubiri Rais Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto hizo wakati wa ziara zake huku wasaidizi wake wapo.

Alisema fedha za kupeleka umeme vijijini ambazo zimechangwa na wananchi, Serikali na wadau wa maendeleo zipo hivyo hakuna sababu ya kukwamisha miradi ya umeme nchini.

Akizungumzia nishati safi ya kupikia alisema Serikali inataka wananchi watumie nishati hiyo na REA wawezeshe upatikanaji wa mitungi ya gesi kwa wananchi.

Alisema Serikali inafanya jitihada za kupata umeme wa kutosha kutoka vyanzo mbalimbali vya umeme ukiwemo mradi wa Bwawa la Julius Nyerere linalotarajiwa kuzalisha Megawati 2115 ambazo zitaongeza umeme kwenye Gridi ya Taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy alisema Mkoa wa Geita una vijiji 461; 399 ambavyo ni sawa na asilimia 86.6 vimepata umeme wa REA, awamu ya tatu, mzunguko kwanza, REA awamu ya pili na REA awamu ya kwanza.

Alisema REA inaendelea kutekeleza miradi ya umeme mkoani Geita na wakandarasi wapo maeneo ya miradi.

Aliitaja miradi inayoendelea kutekelezwa kuwa ni REA awamu ya tatu mzunguko wa
pili, mradi wa kupeleka umeme pembezoni mwa miji awamu ya tatu, mradi
wa kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo pamoja na
mradi wa kupeleka umeme kwenye vituo vya afya na pampu za maji.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya