Friday, March 14, 2025
spot_img

WANA NDUGU WANAODAIWA SIYO RAIA WAPAMBANA

Patricia Kayira

  

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

WANA ndugu wawili, Patricia Kayira na Pamela Kayira wanaodaiwa kuwa siyo raia halali wa Tanzania sasa wameanzisha mapambano ya chini kwa chini ya kuzuia habari zao kuripotiwa.

Katika mapambano hayo wanawatumia baadhi ya watu wanaodai kuwa ni ndugu zao kuzuia kuripotiwa kwa habari zao huku wao wamekuwa wamezuia simu zao za mkononi kupokea wito wa simu au ujumbe mfupi wa maneno kutoka Tanzania PANORAMA Blog.

Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Godfrey kupiga simu na kueleza kuwa kimefanyika kikao cha ukoo wa Kayira kujadili namna taarifa hizo zilivyovuja na namna ya kuzidhibiti zisiendelee kusambaa huku akiomba zisiandikwe tena.

Mtu huyo ambaye baadaye ilibainika alidanganya jina lake kwa sababu uchunguzi ulibaini jina lake halisi ni John Dandi na alitumia simu ya mtu mwingine iliyosajiliwa kwa jina la Godbless Mariki kuwasiliana na Tanzania PANORAMA Blog aliahidi kukutana na waandishi siku inayofuata kueleza ukweli kuhusu utata wa uraia wa Patricia na Pamela jambo ambalo hakulitekeleza na hata alipopigiwa simu na kuahidi kufika, hakutekeleza ahadi yake hiyo.

Wakati hayo yakiendelea, Michael Laiser anayelia kusalitiwa, kuteswa na kutelekezewa watoto na mkewe Pamela ambaye aliibua tuhuma za utata wa uraia wa Patricia na Pamela ameiambia Tanzania PANORAMA kuwa sasa ameanza kutishwa na wana ndugu hao kwa kutoa taarifa zisizo sahihi dhidi ya baba mzazi wa wana ndugu hao.

Laiser amesema kuwa taarifa yake ya awali kuhusu baba wa wana ndugu hao ama ilikosewa kuripotiwa au alikaririwa vibaya kuwa mzee huyo, Barthlomew Samson Kayira alikwishafariuki dunia wakati uhalisia ni kwamba bado yupo hai isipokuwa mkewe, Christina Pallagyo ndiye aliyafariki dunia.

“Naona mapambano yameanza sasa wananitishia kunishtaki kwa kukosea ile taarifa kuhusu baba yao. Kama nilivyowaambia baada ya kuandika kuwa huyo mzee yupo hai ila mkewe ndiyo alishafariki. Badala ya kujibu kuhusu uraia wao wanataka kujificha kwenye huko kukosea taarifa lakini mimi sina tatizo wakashtraki tu,” alisema Laiser

Katika madai yake, Laiser anawatuhumu mkewe Pamela na Patricia ambaye ni mfanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe kufanya udanganyifu na kughushi uraia na anamtaja Patricia kuwa chanzo cha kusambaratika kwa ndoa yake.

Patricia Kayira

 

Awali akiongea na Tanzania PANORAMA Blog, Patricia alisema yeye ni raia halali wa Tanzania na amezaliwa na wazazi wote wawili, baba na mama watanzania na kwamba Laiser ameamua kumchafua baada ya kuona anamsaidia mkewe ambaye ameshindwa kumtunza.

Wiki iliyopita Tanzania PANORAMA Blog iliripoti kuwa mgogoro unaodaiwa kusababishwa na usaliti wa mapenzi ndani ya ndoa ya wanandoa Michael Laiser na Pamela Kayira umesababisha watoto wao kukosa haki ya malezi bora.

Laiser  ndiye aliyefichua kuwepo kwa hali ya hofu na wasiwasi ndani yanfamilia yake katika mahojiano aliyoyafanya na Tanzania PANORAMA Blog hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine alimtuhumu mkewe kuwa chanzo cha kuwepo kwa hali hiyo kutokana na vitendo vyake vya kusaliti penzi lao na kuwatelekeza watoto wao.

Katika mahojiano hayo, Laiser alimtuhumu Pamela kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamume mwingine, kuipa kisogo familia yake, (mumewe Laiser na watoto wao watatu), kuwa na kiburi na jeuri, kuondoka nyumbani asubuhi kwenda kazini na kurudi asubuhi ya siku inayofuata akiwa hajulikana alikolala huku akijua kuwa uraia wake pamoja na wa dada yake ni wa mashaka pamoja  na kuhama nyumbani kwake kwa muda wa miezi sita kwenda kuishi mahali kusikojulikana.

Laiser alisema amemgundua mkware mwenye uhusiano wa kimapenzi na mkewe na anamuomba amuonee huruma kwa sababu kitendo anachokifanya kina athari mbaya katika maisha ya watoto wake na kinaiharibu familia yake. Pia alimuomba mwajiri wa mkewe asaidie kuokoa ndoa yake na watoto kupata mapenzi na malezi ya mama yao.

Kwa upande wake Pamela alizipuuza tuhuma hizo. Katika mahojiano aliyofanya na Tanzania PANORAMA Blog, Pamela alikataa kutoa ushirikiano na aliikana ofisi anayofanyia kazi, Taaisi ya Chakula na Lishe.

Wakati Pamela akipuuza tuhuma na kilio cha mumewe, bosi wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dk. Germana Henry Leyna naye alikataa kuthibitisha kama Pamela ni mfanyakazi wa taasisi anayoiongoza au lah na alijiweka mbali na ombi la Laiser la kumkalisha kitako Pamela kumsihi kuijali familia yake na hasa kulea watoto wake.

 

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya