Thursday, March 13, 2025
spot_img

MBIVU, MBICHI ZA ANAYETUHUMIWA KUUZA UMEME KWA ULANGUZI KUJULIKANA JUMATATU

Ugur Gurses anayetuhumiwa na EWURA kufanya biashara ya kuuza umeme bila kuwa na leseni ya mamlaka hiyo na kuuza kwa bei ya juu

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

KITENDAWILI cha tuhuma zinazomkabili mfanyabiashara Ugur Gurses za ulanguzi wa umeme, kufanya biashara ya umeme bila kuwa na leseni ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kinatarajiwa kuteguliwa jumatatu, Oktoba 25, 2021

Gurses pia anadaiwa kukataa kupokea karipio la kisheria la EWURA la kutojihusisha na vitendo vya uvunjivu wa sheria,.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Dar es Salaam (PRO), Pius Hilla katika mahojiano yake na Tanzania PANORAMA Blog iliyotaka kujua iwapo shauri lenye tuhuma hizo limekwishafikishwa kwake, hatua zilizofikiwa kulishughulikia na mashtaka atakayofunguliwa Gurses kutokana na tuhuma zinazomkabili.

Katika majibu yake, Hilla alisema shauri hilo halijafika mikononi mwake lakini analifuatilia kwenye ofisi za mikoa zinazounda Kanda ya Dar es Salaam ili lifikishwe kwake na kuahidi kuwa mpaka jumatatu mchana atatoa kauli yake.

“Iko hivi, unajua tangu mwezi August mwaka huu, DPP aliunda mikoa ya kimashtaka, kuna ofisi za mashtaka za mikoa ya Kinondoni, Ilala na Temeke. Hizi zinaunda Kanda ya Dar es Salaam na mimi ni kiongozi wa kanda. Sasa hapa mikononi mwangu hilo faili halijafika.

“Naomba muda nifuatilie, acha nifuatilie lipo wapi hilo faili. Wewe naomba nitafute jumatatu mchana nitakuwa na jibu, nitatoa kauli jumatatu kuhusu suala hili,” alisema Hilla.

Awali, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu alipozungumza na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu suala hilo alisema anafuatilia faili la shauri la mfanyabiashara Gurses ambalo lilikuwa halijafika mezani kwake.

DPP Mwakitalu alisema upo uwezekano faili hilo liliwasilishwa katika ofisi ya kanda na alielekezaTanzania PANORAMA Blog kuwasiliana na ofisi hiyo kujua kama lilipokelewa huko na namna lilivyofanyiwa kazi.

“Faili la shauri hilo halijafika ofisini kwangu, inawezekana EWURA waliliwasilisha katika ofisi za kanda, haya mambo mengine yafanyika huko ofisi za kanda lakini nakushukuru umeniambia, nalifuatilia,” alisema DPP Mwakitalu.

EWURA inamtuhumu Gurses, raia wa Uturuki ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Adamas Group yenye ofisi zake Karioakoo, Dar es Salaam inayojihusisha na biashara ya nyumba kufanya biashara ya umeme kinyume cha sheria akiwa hana leseni ya mamlaka hiyo na kuuuza kwa bei ya juu.

Meneja Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa Gurses ana makosa mawili, la kwanza ni kuuza umeme bila kuwa na leseni ya EWURA na kosa la pili ni kuuza umeme kwa bei ya juu.

Alisema EWURA baada ya kubaini makosa hayo kwa Gurses ilimpelekea karipio la kisheria lakini alikataa kulipokea hivyo imelifikisha shauri hilo kwa DPP ambaye ana nguvu za kisheria na pia ana vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

“Huyu mtu ana makosa yafuatayo, 1) kuuza umeme wakati hana leseni ya EWURA, 2) kuuza umeme kwa bei ya juu. Tulimpelekea ‘complaince order’ karipio la kisheria na alikataa kupokea.

“Katika hali kama hii, sheria inatutaka tumpelekee DPP ambaye ana vyombo vya dola kama polisi ili ampeleke mahakamani. DPP analifanyia kazi na tumeishakaa na DPP juu ya hili shauri.

“Tunasubiri hatua za DPP. DPP ana taratibu zake na anaweza kufanya uchunguzi kabla ya kuchukua hatua. Sasa fuatilia kwa DPP ‘unless’ DPP aamue kuwa hana nia ‘but’ itakuwa fundisho,” alisema Kaguo.

 

 

   

   

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya