Monday, December 23, 2024
spot_img

SERIKALI KUFYEKA KODI UTALII WAGENI WAKIMIMINIKA MBUGANI

RIPOTA PANORAMA

SERIKALI imependekeza marekebisho ya ada na tozo mbalimbali katika sekta ya utalii ili kuwapunguzia gharama watalii wanaotembelea vivutio vilivyopo nchini.

Tofauti na tetesi na taarifa zinazozua mijadala sasa hususan kwenye baadhi ya makundi sogozi kuhusu makali ya kodi kwenye utalii, hotuba rasmi ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2023/24, iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba Juni 15, 2023 bungeni, jijini Dodoma, ilipendekeza kufuta na kupunguza baadhi ya ada na tozo ili kutoa mwanya kwa sekta hiyo kupumua zaidi.

Akisoma bajeti hiyo, Dk. Nchemba alilitaja eneo la kwanza ambalo Serikali imependekeza kufanyiwa marekebisho kuwa ni kufuta ada ya kupanga na kurudia kupanga huduma za malazi zilizo nje na ndani ya maeneo ya hifadhi.

Dk. Nchemba alisema, Serikali inapendekeza pia kupunguiza ada ya leseni ya biashara ya utalii katika huduma za malazi zinazomilikiwa na Watanzania, kutoka Dola za Marekani 2,500 hadi Dola za Marekani 1,500 kwa hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

Pia alisema kuwa, pendekezo hilo linazigusa hoteli zenye hadhi ya nyota nne, zinazolipa ada ya leseni Dola za Marekani 2,000 na badala yake zilipe Dola za Marekani 1,000 na kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tatu zinazolipa ada ya leseni Dola za Marekani 1,500, sasa zilipe Dola za Marekani 500.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba akisoma Bajeti ya Serikali bungeni, Dodoma Juni 15, 2023.

Dk. Nchemba alisema, kwa hoteli zenye hadhi ya nyota mbili zinazolipa Dola za Marekani 1.300 sasa zilipe Dola za Marekani 300 huku zile zenye hadhi ya nyota moja, zinazolipa Dola za Marekani 1,000 zilipe Dola za Marekani 200.

“Kupunguza ada ya leseni ya utalii kwa huduma za malazi ambazo hazijakaguliwa na kupangwa katika viwango vya ubora nje ya maeneo ya hifadhi kutoka Dola za Marekani 1,000 hadi kufikia Dola za Marekani 300, huduma za malazi zinazopatikana katika makazi ya mtoa huduma kutoka Dola za Marekani 400 hadi Dola za Marekani 100 na hosteli kutoka Dola za Marekani 400 hadi Dola za Marekani 100,” alisema Dk. Nchemba wakati akiwasilisha hotuba yake hiyo bungeni.

Aidha, Dk. Nchemba alisema licha ya athari za kiuchumi zilizosababishwa na ugonjwa wa UVIKO 19 kuwa kubwa duniani kote, kazi iliyofanywa na Rais Samia, kutengeneza filamu inayojulikana kwa jina la The Royal Tour iliipa uhai sekta ya utalii kwa kuvuta watalii wengi na kuongozeka kwa ujazo wa makusanyo kwenye kapu la mapato yatokanayo na utalii.

“Mafanikio hayo ni ongezeko la idadi ya watalii wa nje kutoka 992,692 mwaka 2021 hadi watalii 1,454,920 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 57.7.

“Aidha, watalii wa ndnani waliotembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini walikuwa 2,363.260, ikilinganishwa na watalii wa ndani 788,933 waliotembelea vivutio vya utalii mwaka 2021,” alisema Dk. Nchemba.

Dk. Nchemba alisema ongezeko hilo la watalii limeongeza mapato ya sekta ya utalii kutoka Dola za Marekani milioni 1,310 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani 2,527.7 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 93.   

.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya