Wednesday, December 25, 2024
spot_img

ULAWITI WA DIWANI RAIBU WAISIKITISHA CCM KILIMANJARO

Diwani wa Kata ya Bomambuzi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini mkoani Kilimanjario, Juma Raibu (mwenye suti nyeusi) akiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya kijana anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Bondeni Lounge, Februari mwaka jana.

RIPOTA PANORAMA

Moshi, Kilimanjaro

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro kimeeleza kusikitishwa na tuhuma zinazomuandama Diwani wa Kata ya Bomambuzi, Juma Raibu zikimuhusisha na kauli za kutaka kuwalawiti madiwani wenzake.

Mwenyekti wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjato, Patrick Boisafi ameiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa chama hicho kinalaani vitendo vya ushoga, ulawiti na vingine vyote vinavyokinzana na maadili ya kitanzania.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA leo kwa njia ya simu, Boisafi amesema tuhuma zinazomuandama Diwania Raibu zinakisikitisha chama hicho na kwamba iwapo zitafikishwa rasmi ndani ya chama kwa mara pili na kubainika kuwa ni za kweli, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

“Hizi tuhuma siyo mpya ziliibuka tangu mwaka jana. Huyu Raibu alikuwa Meya lakini akatuhumiwa kwa hayo mambo pamoja na mengine na uchunguzi ukafanyika ikabainika ni tuhuma za kweli hivyo akaondolea kwenye umeya akabaki kuwa diwani.

“Kwa hiyo hatua zilichukuliwa dhidi yake. Lakini kama bado anaendelea na mwenendo huo, kwa kweli chama kinasikitishwa sana na tabia hizo za mambo ya ushoga na iwapo tuhuma zitakuja rasmi kwa mara nyingine na ikabainika bado anajihusisha na matendo hayo ya aibu, hatua kali sana zitachukuliwa na chama.

“Mimi niko Dar es Salaam sina taarifa kama kuna tuhuma mpya za aina hiyo zinazomuhusu tena Diwani Raibu na hapa ninajiandaa kusafiri kesho nakwenda nje ya nchi hivyo inawezekana kuna tuhuma zimewasilishwa ofisini mimi sijui lakini mtafute katibu, yeye yuko huko Moshi atakwambia kama kuna tuhuma mpya, lakini ninachosema, safari hii CCM itachukua hatua kali sana kwa vitendo vya aina hiyo kama huyo Raibu kavifanya tena,” alisema Mwenyekiti Boisafi.

Tanzania PANORAMA Blog imemtafuta bila mafanikio Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro ili kuzungumzia hilo, hata hivyo jitihada za kumpata bado zinaendelea.

Diwani Raibu aliondolewa kwenye wadhfa wa umeya Agosti 11, mwaka jana baada ya kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye na madiwani 20 kati ya 30 wa baraza hilo akituhumiwa kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya kijana anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Raibu alihudhuria sherehe hiyo iliyofanyika kwenye Mgahawa wa Bondeni Lounge, Februari 13, mwaka jana na baadaye picha zake akiwa kwenye tikio hilo zilisambaa mitandaoni, moja ya picha hizo ilimwonyesha akilishwa keki na kijana huyo ambaye alikuwa amevaa heleni kwenye masikio yake. 

Akiwa kwenye sherehe hizo, Raibu anadaiwa kupokea ‘kilio’ cha mashoga hao na kuahidi kukipatia ufumbuzi; mashoga hao inadaiwa pamoja na mambo yao mengine, ‘walilia’ kutotambuliwa kwa haki zao za ushoga.

Mbali na hilo, Raibu pia alikuwa akituhumiwa kutumia madaraka yake vibaya, rushwa katika utoaji wa vibali vya ujenzi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kufanyika shughuli za ujenzi wa majengo ya chini.

Katika mlolongo wa tuhuma zilizokuwa zikimuandamana ilikuwemo pia ya kutoa maamuzi ambayo hayajaidhinishwa na baraza la madiwani, kutowaheshimu wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala na kutoruhusu mjadala kuhusu vikundi vilivyoomba mikopo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya