Monday, December 23, 2024
spot_img

RAIS SAMIA LEO ‘KUHEMEA’ MAGOLI YA SIMBA KWA MILIONI 5

RIPOTA PANORAMA

RAIS Samia Suluhu Hassan, leo atanunua kila goli litakalofungwa na Timu ya Simba Sports Club (SSC) kwa Shilingi milioni tano itakapokuwa ikimenyana na Timu ya Raja Casablanca ya Morocco kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kama hiyo haitoshi, kesho Jumapili, Rais Samia atafungua tena pochi yake kununua kila goli litakalofungwa na Timu ya Yanga itakapoingia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Timu ya TP Mazembe ya DR Congo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Uamuzi wa Rais Samia kubeba kiasi hicho kikubwa cha noti kwenda kununua magoli yatayofungwa na Timu ya Simba leo ulitangazwa kwa umma mapema wiki hii na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Gerson Msigwa.    

“Rais Samia amenituma nisema kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga, ametangaza kulinunua kwa Shilingi milioni tano. Kazi kwenu wachezaji, ukifunga magoli mawili una Shilingi milioni 10. Lengo lake pamoja na kufunga magoli timu zetu lazima zishinde kwenye michuano hii,” alisema Msingwa.

Timu ya Simba SC inahitaji ushindi katika mchezo wake wa leo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri na kufuzu kucheza robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kupoteza kwa tabu mchezo wake wa kwanza wa kundi C dhidi ya timu ya Horoya AC ya Guinea, Jumamosi iliyopita.

Mshambuliaji hatari wa Timu ya Simba Sports Club, Pape Sakho akifunga bao bora Afrika mwaka. Sakho leo anatarajiwa kuendeleza makali yake.

Wakati Simba SC ikihitaji ushindi leo unaochangizwa na uamuzi wa Rais Samia kuwamwangia noti za kutosha wachezaji wataofunga magoli, kesho Timu ya Yanga itahitaji ushindi kwa udi na uvumba ili kujiweka katika nafasi ya kucheza robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya