Saturday, July 19, 2025
spot_img

SAFARI YA MWISHO YA PAPA BENEDICTO XVI DUNIANI

VATICAN

PAPA Mstaafu Benedicto XVI, Alhamis ya Januari 5, 2023 mwili wake ulizikwa kwenye kaburini lililo katika kanisa la Mtakatifu Petro, Vatican.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vya Vatican na Italia, Hayati Papa Benedicto XVI ambaye jina lake halisi ni Joseph Ratzinger, mwili wake ulizikwa katika kaburi ambalo hapo awali, mwili wa Hayati Papa John Paulo II ulizikwa kabla ya mabaki ya mwili wake kuhamishiwa sehemu nyingine ndani ya Kanisa la Mtakatifu Petro.

Ibada ya misa ya mazishi ya Hayati Papa Benedicto XVI iliyongozwa na Papa Francis ilifanyika kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro na kuhudhuriwa na waumini zaidi ya 50,000.

Miongoni waliohudhuria mazishi hayo ni ujumbe mkubwa uliotoka Jimbo la Bavaria la Ujerumani, ambako ndiko asili ya Hayati Papa Benedicto XVI. Ujumbe huo ulisafiri kutoka Ujerumani kwenda Roma kushiriki ibada hiyo ya mazishi.

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, Rais wa nchi hiyo, Frank-Walter Steinmeier, Kiongozi Mkuu wa Jimbo la Bavaria, Markus Söder pamoja na wanasiasa wengine mashuhuri kutoka Ujerumani walihudhuria ibada ya mazishi ya Hayati Papa Benedicto XVI.

Akitoa salamu za rambirambi, Rais Steinmeier alimtaja Hayati Papa Benedicto XVI kuwa mwanateolojia bora na mwenye unyenyekevu mkubwa na kwamba kujiuzulu kwake wadhfa wa upapa mwaka 2013 hakukuondoa heshima aliyokuwa nayo duniani kote. Hayati Papa Benedicto alikuwa Papa wa kwanza wa Kanisa Katoliki kujiuzulu katika kipindi cha miaka 600.

Naye Papa Francis ambaye aliongoza ibada hiyo ya mazishi alimwelezea Hayati Papa Benedicto XVI kwa kusema; “Tukizingatia kauli ya mwisho ya bwana na ushuhuda wa maisha yake yote, sisi pia, kama jumuiya ya kanisa tunahitaji kufuata nyayo zake na kumkabidhi ndugu yetu mikononi mwa Baba. Taa ziangazie mikono hiyo ya rehema kwa mafuta ya Injili ambayo aliionyesha na kuieneza katika maisha yake yote.”

Mapema Alhamis kabla ya kuanza kwa ibaa ya mazishi yake, Vatican ilitoa historia rasmi ya maisha ya Hayati Papa Benedict XVI katika hati fupi iliyoandikwa kwa Lugha ya Kilatini; inayofahamika zaidi kwa jina la ‘rogito’ ambayo iliwekwa katika jeneza lake kabla ya kufungwa pamoja na sarafu na medali zilizotengenezwa wakati wa uongozi wake.

Baada ya mazishi ya Hayati Papa Benedicto XVI, umati wa watu uliohudhuria ulipiga kelele kwa Lugha ya Kiitaliano ukisema ‘Santo Subito’ ikimaanisha kuwa ulitaka Hayati Papa Benedict XVI atangazwe mtakatifu. Tukio kama hilo lilipata kutokea wakati wa mazishi ya Hayati Papa John Paul II.

Rekodi zilizopo zinaonyesha mapapa watatu kati ya watano wa miaka ya hivi karibuni ndio waliotangazwa kuwa watakatifu, Hata hivyo, karibu theluthi moja ya mapapa wote waliopata kuliongoza Kanisa Katoliki kwa kipindi cha miaka 2,000 ya uhai wa Kanisa Katoliki duniani walikwishatangazwa kuwa watakatifu.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya