Tuesday, December 24, 2024
spot_img

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMTEMBELEA LOWASSA HOSPITALINI

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesafiri kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kumtembelea na kumjulia hali Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amelazwa hospitalini nchini humo akipatiwa matibabu.

Waziri Mkuu Majaliwa amekwenda Afrika Kusini Disemba 28, 2022 kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan na sambamba na kumjulia hali Lowassa, amekutana na familia ya Lowassa na kuipatia salamu za pole kutoka kwa Rais Samia.

Akiwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Rais Samia anafuatilia mwenendo wa hali ya afya ya Lowassa kwa karibu na anamuombea afya njema.

Akizungumza baada ya kupokea salamu za Rais Samia, Mke wa Lowassa, Regina Lowassa alimshukuru Rais Samia kwa kuwa karibu na familia yake na kwa namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mume wake.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya