Tuesday, December 24, 2024
spot_img

WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE BUKOBA KUAGWA LEO

RIPOTA PANORAMA

MIILI ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Precision Air iliyotumbukia Ziwa Victoria jana asubuhi inatarajiwa kuagwa leo katika Uwanja wa Kaitaba.

Taarifa zilizopatikana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera zimeeleza kuwa shughuli ya kuaga miili hiyo itafanyika majira ya asubuhi na tayari miili 18 imekwishatambuliwa.

Jana, baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufika mkoani Kagera na kukagua eneo la ajali alisema idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni 19.

Taarifa zilizokusanywa na Tanzania Panorama Blog kuhusu ajali hiyo zimeonyesha kuwa ilikuwa ikisafiri kutoka Dar-es-Salaam kuelekea Mkoa wa Kagera na ilipata hitilafu muda mfupi kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ndege hiyo yenye namba za usajili 5hpwf ilikuwa watu 43, kati hao 39 walikuwa abiria, wawili wahudumu na marubani wawili.

Taarifa iliyotolewa awali na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ilieleza kuwa watu 26 waliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa matibabu.

Taarifa za hivi karibuni zimeeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitokea Dat es Salaam kwenda Mkoa wa Kagera na ilipata hitilafu na kuanguka Ziwa Victoria majira ya saa 2:27asubuhi ikiwa mita 100 kutoka uwanja wa ndege Bukoba.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya