Sunday, August 24, 2025
spot_img

LOLIONDO KULINDWA USIKU NA MCHANA,, MIPAKA YAKAMILIKA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Mkoa wa Arusha alipokuwa akikagua kazi ya uwekaji mipaka katika eneo la Loliondo, Ngorongoro jana.


●Vigingi 424 vyawekwa kama alama

●Barabara ya kilomita 108 yachongwa mpakani

●Kigingi namba moja maalumu kumkumbuka askari aliyepoteza maisha.

MWANDISHI MAALUM, LOLIONDO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana alitangaza kukamilika kwa kazi ya uwekaji wa alama za mipaka katika Pori Tengefu la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha.

Akizungumza jana baada ya kukagua eneo la Kilomita 1,500 zilizowekewa mipaka katika eneo la Ngorongoro, Waziri Mkuu Majaliwa alipongeza wote walioshiriki kufanya kazi ya kuweka mipaka na kuwataka wananchi kuepuka taarifa hasi na za upotoshaji kuhusu eneo hilo.

Alisema kazi hiyo imefanyika kwa nia njema ya kuhifadhi eneo hilo na hakuna mwananchi yoyote aliyehamishwa kwa nguvu katika eneo hilo.

“Eneo hili ni muhimu kwa kuwa lina vyanzo vya maji na mazalia ya nyumbu ambayo ni muhimu kwa uwepo wa maeneo ya Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro,” alisema Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alibainisha eneo la Ngoronforo litaendelea kulindwa wakati wote ili kuhifadhi eneo hilo ambalo ni muhimu kwa uhifadhi kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii Pindi Chana alisema wizara na taasisi zilizo chini yake wataendelea kusimamia maeneo yote ya uhifadhi kwa niaba ya wananchi.

Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema kazi ya kuweka mipaka imekamilika kwa wakati na kwa mafanikio makubwa. Mongella ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha na msimamizi wa kazi hiyo, alisema Askari Garlus Mwita aliyepoteza maisha akiwa katika kazi ya kujenga mnara atapewa heshima kwa kigingi namba moja kupewa jina lake kama alama ya kumuenzi.

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ALIYOIFANYA JANA LOLIONDO, NGORONGORO


 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya