Monday, December 23, 2024
spot_img

WABUNGE 19 WACHAGULIWA KUONGOZA KAMATI ZA BUNGE

 

NA CHARLES MULLINDA

WABUNGE 19 wamechaguliwa kuwa wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge na wengine 19 wamechaguliwa kuwa makamu wenyeviti wa kamati hizo.

Wabunge hao waliochaguliwa mapema wiki hii ni David Mwakiposa Kihenzile, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mohamed Omary Mchengerwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Mussa Azzan Zungu aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hamphery Hezron Polepole, Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Stanslaus Haroon Nyongo, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Atupele Fredy Mwakibete. Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

Wengine ni Dunstan Luka Kitandula, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Moshi Selemani Kakoso. Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Dk. Aloyce Andrew Kwezi, Mwenyekiti Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Dk. Christine Gabriel Ishengoma, Mwenyekiti Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Kamati ya Hesabu za Serikali, Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Naghenjwa Kaboyoka, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mwenyekiti ni  Grace Victor Tendega, Kamati ya Masuala ya Ukimwi Mwenyekiti ni Fatma Hassan Toufig na Kamati ya Bajeti Mwenyekiti ni Sillo Daniel Baran.

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Kinga Na Madarasa ya Bunge ni Emmanuel Adamson Mwakasaka.

Makamu wenyeviti waliochaguliwa ni Eric Shigongo, Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Najma Murtaza Giga, Katiba na Sheria, Vincent Paul Mbongo, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Abdallah Jafari Chaurembo, Utawala na Serikali za Mitaa na Aloyce John Kamamba, Huduma na Maendeleo ya Jamii.

George Nataly Malima, Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Seifa Khamis Gulamali, Nishati na Madini, Anna Kilango Malecela, Miundombinu, Dk. Spephen Chaya, Ardhi, Maliasili na Utalii, Athuman Almasi Maige, Kilimo, Mifugo na Maji, na Japhet Hasunga, Hesabu za Serikali.

Selemani Jumanne Zedi, Hesabu za Serikali za Mitaa, Dk Alice Karungi Kaijage, Masuala ya Ukimwi, Omar Mohamed Kigua, Bajeti, Stela Alex Ikupa, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Ridhiwan Kikwete, Sheria Ndogo.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya