Monday, December 23, 2024
spot_img

BUNGE LAKOSHWA NA UTENDAJI WA RITA

RIPOTA PANORAMA

KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria imepokea na kuridhishwa na taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Akitoa pongezi juzi jijini Dodoma leo Oktoba 30, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mhagama amesema RITA imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake na kufanyia kazi maagizo ya Kamati hiyo ambayo ni pamoja na kuboresha huduma Kwa njia ya kidigitali na kutoa huduma bora.

Ameongeza kuwa Kamati yake inafahamu mafanikio kadhaa yaliopatikana katika Usajili wa vizavi na vifo, ndoa na talaka, usajili wa bodi za wadhamini na huduma ya kuandika na kuhifadhi wosia, licha ya changamoto za upungufu wa rasilimali watu na fedha.

“Napenda kuipongeza RITA kwa kutushirikisha kwa ukaribu katika kila hatua ya utekelezaji wa majukumu yake na sisi kama wabunge tunafahamu mafanikio na changamoto zinazoikabili RITA,” amesema Mhagama.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro ameishukuru kamati hiyo kwa kuwa karibu na wizara na taasisi zake zote kusimamia na kutoa mapendekezo yaliyowezesha kufanikiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Aidha, Dk Ndumbaro amesema Serikali inatambua umuhimu wa huduma zinazotolewa na RITA kwani zinagusa maisha ya kila mwananchi pamoja na usalama wa Nchi kwa ujumla.

“Tunatambua kama Wizara yenye dhamana ya kuisimamia RITA kila jukumu linalofanywa na taasisi hii ni muhimu, kwa mfano usajili wa vizazi na vifo tunapata takwimu kwa ajili ya mipango ya maendeleo.

Hivyo hivyo usajili wa bodi za wadhamini, ufilisi, kuasili watoto, ndoa na talaka, zote hizo zinagusa maslahi ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake,” amesema Dk Ndumbaro.

Waziri huyo ameiambia Kamati hiyo ya Bunge kuwa hivi karibuni Tanzania iliwakilishwa na Kabidhi Wasii Mkuu, Angela Anatory katika kikao cha wataalam wa masuala ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu Barani Afrika kilichofanyika Oktoba 24 – 28, 2022 Jijini Addis Ababa Ethiopia.

Naye Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa RITA, Angela Anatory kupitia taarifa aliyowasilisha mbele ya Kamati ya Bunge amesema katika utoaji wa huduma za usajili wa vizazi na vifo, ndoa na talaka pamoja na bodi za wadhamini, Wakala umeboresha na Sasa huduma hizo zinatolewa Kielektroniki kupitia e –Huduma.

Amsema kupitia huduma hiyo, mwananchi anaweza kutuma maombi ya huduma anayotaka Kisha kujibiwa ndani ya muda mfupi badala ya kufika Moja kwa Moja katika ofisi za RITA.

Kwa upande wa Usajili watoto wa umri chini ya Miaka mitano Bi. Anatory amesema tayari Mikoa 23 inatekeleza mpango huo ambapo watoto wanasajili na kupatiwa vyeti vya Kuzaliwa bure katika vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya mama na mtoto na ofisi za Watendaji Kata.

Ameongeza kuwa kupitia mpango huo Serikali imefanikiwa kupata taarifa Kwa wakati za watoto wapatao 8,106,469 katika Mikoa 23, Halmashauri 163 kata 3,522 na vituo vya Afya 6,320.

“Teknolojia ya simu za mkononi imetuwezeaha kutuma taarifa kutoka katika vituo vya Usajili hadi kwenye Kanzi data ya RITA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam tofauti na zamani ilikuwa taarifa hivyo tusafirishe kwenye basi au Magari ya mizigo hivyo kuchelewa kufika kwa wakati”. Alisema Anatory.

Wakati huo huo ameihakikishia Kamati hiyo ya Bunge kutekeleza maagizo yote yakiwemo kuwafuata Wananchi sehemu wanakoishi na kuwapatia huduma pamoja na kuimarisha zaidi mifumo ya TEHAMA ili huduma zote zitolewe Kielektroniki.

RITA imewasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa majukumu ya kila simu pamoja na maagizo ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ambapo kila mwaka hufanya hivyo na kupimwa uwajibikaji wake katika utoaji wa huduma Kwa Wananchi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya