Tuesday, December 24, 2024
spot_img

Tajiri azungumzia wizi wa tanzanite Mirerani


Na Mwandishi Wetu


MMOJA wa wakurugenzi wa Kampuni ya Sky Associates Limited, Faisal Juma Shahbhai, amesema kuingia katika maeneo ya uchimbaji madini ya tanzanite yanayomilikiwa na kampuni yake na kushiriki kwenye uchejuaji ni haki yake.
Amesema madai ambayo anaelekezewa na washirika wake wa kibiashara kuwa alihusika kutorosha kwa ndoo madini ya tanzanite, hayana msingi na amewataka wenye ushahidi wautoe hadharani ili autolee majibu.

Shahbhai aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, siku chache baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti taarifa za utoroshwaji wa ndoo ya madini hayo huku jina lake likitajwa kuhusika.
Alisema taarifa kuwa alikuwa mgodini siku ambayo madini hayo yanadaiwa kutoroshwa ni za kweli, lakini alikuwa eneo hilo kwa sababu shughuli zake zinamruhusu kwenda kukagua madini na kushiriki kuyachenjua. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Sky Associates Limited, Faisal Juma Shahbhai

“Hiyo ndiyo kazi yetu sisi, mimi kuwa maeneo hayo na kuwa na madini ni sawa kabisa, kati ya tarehe 19 au 20 ni kweli nilikuwa kwenye shughuli ya uchenjuaji wa madini. Kuwa katika maeneo yangu ya kazi ya kuchenjua madini si jambo la ajabu kwangu kwa sababu ndiyo shughuli zangu,” alisema Shahbhai.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za kuandamana na mdogo wake anayetajwa kwa jina la Arafat na mmoja wa wafanyakazi wake anayetajwa kwa jina la Yusuf Mhagama, kuingia ndani ya chumba cha uchenjuaji, alisema taarifa hizo ni kweli.

“Ni kweli Arafat ni mdogo wangu wa damu, kuna mambo mengi ya msingi yanayoweza kujenga taifa ya kuandika huku Mirerani badala ya haya ya uongo uongo,” alisema Shahbhai. 

Hata hivyo, alikanushan taarifa kuwa Arafat na Mhagama waliondoka eneo la mgodi wakiwa na ndoo yenye madini ya tanzanite yanayodaiwa kutoroshwa na kwamba wakiwa njiani kuelekea mjini Arusha walibadilisha gari.

“Yaani gari iende ibadilishwe huko iweje sasa, kwa nini mtu hata kama anataka kitu asiende na gari hiyo hiyo? Watanzania hawajui kitu, hawajui kabisa biashara ya tanzanite, wako ‘very blind’ kwenye biashara hiyo.

“Tunapowaambia vitu, tuwaambie ambavyo kesho hata mwenyezi Mungu akisimama tuweze kusimama kujibu kwamba Mola nilichokisema kiko sawa. Yupo mwandishi alikuja Mirerani kufuatilia suala hili na alikaa hapa kwa muda wa siku tatu, lakini nilimshauri aandike vitu ambavyo vitasaidia jamii ya Watanzania.

“Ni jambo jema kama waandishi wa habari watakuwa wanawajuza watu vitu ambavyo vitajenga uchumi wa taifa kwa sababu hizo taarifa hazijakaa vizuri sana. Katika biashara hii tuna tofauti kubwa na wafanyabiashara wenzetu. 

“Baada ya kuingia kwenye uwekezaji wa biashara ya tanzanite, tumekuwa na ugomvi mkubwa na wachimbaji wadogo kwa sababu maeneo mengi wanayochimba walikuwa wanachimba upande wetu. Nakuhakikishia jambo hilo si la kweli, ni fitina tu,” alisema Shahbhai.

Kauli hii ya Shahbhai imekuja baada ya kuripotiwa kuwa vigogo wa Kampuni ya Sky Associates Limited walihusika na utoroshaji wa madini ya tanzanite yenye thamani ya mabilioni ya shilingi kutoka katika mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mererani mkoani Manyara.

Kwamba Shahbhai na wenzake walitekeleza mpango huo Juni 21 kwa kuyasafirisha madini hayo kwa kutumia gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 710 BWT ambalo ni mali ya Kampuni ya TanzaniteOne, lililokuwa likiendeshwa na Mhagama.
Taarifa zilidai kuwa Mhagama ambaye alikuwa ameambatana na Arafat katika safari hiyo, waliyashusha madini hayo kabla ya kufika Arusha mjini na kuyapakia kwenye gari jingine aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 492 BSS.

Mikito Blog inaendelea na uchungizi wa sakata hili.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya