Tuesday, December 24, 2024
spot_img

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA MAFUNZO KWA VIJANA


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu, Anthony Mavunde akizungumzawakati wa ufunguzi wa mafunzo ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu, Anthony Mavunde amezindua mafunzo ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi kwa vijana 847 wa mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam.
Akizindua mafunzo hayo mkoani Mtwara, Naibu Waziri Mvunde aliwataka vijana kuchangamkia fursa badala ya kusubiri serikali itoe matangazo, au kuwatafuta kwa ajili ya kuwapatia ujuzi. 
“Msingi wa maisha ya kijana unaanzia hapa, kijana wa kitanzania jiamini, timiza wajibu wako. Vijana mliopata fursa ya kuingia kwenye mafunzo haya itumie vizuri fursa hii. Muwe waaminifu na wawajibikaji.
“Acheni tamaa, tambueni kuwa ni kaburi peke yake watu huanza kuchimba toka juu kwenda chini lakini maisha yananzia chini kwenda juu,” alisema Naibu Waziri Mavunde.
Alisema mafunzo ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi yanatolewa na serikali hivyo vijana  wahakikishe wanatumia vizuri fedha zinazotolewa katika mafunzo.
Tatarifa ya Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu. 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya