Tuesday, December 24, 2024
spot_img

RC MAKONDA AKABIDHIWA PIKIPIKI ZA MILIONI 400


KAMPUNI ya TONGBA ya China inayojihusisha na utengenezaji pikipiki, leo imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pikipiki 10 za kisasa.
Pikipiki hizo zenye thamani y ash. Milioni 400 ni maalumu kwa ajili ya kutumiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo jijini Dar es Salaam, Makonda alisema aliiomba TONGBA msaada wa pikipiki za kisasa kwa ajili kwa ajili ya askari wa usalama barabarani ili kukiongezea uwezo kikosi hicho katika utekelezaji wa majukumu yake.
Alisema kupatikana kwa pikipiki hizo kutaongeza ufanisi wa utendaji kazi wa askari wa usalama wanapoongoza misafara ya viongozi, misiba na kuwahisha wagonjwa waliozidiwa hospitalini.
“Lengo langu ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi, natamani kuona askari wana vifaa vya kutosha. Hadi sasa tumepata baiskeli 500, pikipiki za kawaida 200, kompyuta 100 , pikipiki kwa ajili ya askari wa  usalama barabarani na matengenezo ya magari,” alisema Makonda. 
Wakati huo huo, Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata askari wote waliobainika kushirikiana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya na wanaobambikia wananchi kesi ndani ya muda wa saa tano.
Agizo hilo la Makonda limekuja baada ya juzi kupatiwa taarifa za mmoja wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aliyekuwa mikononi mwa polisi kutoweka katika mazingira yasiyoeleweka.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, muuza unga huyo baada ya kutoweka mikononi  mwa polisi alirudi katika hoteli aliyokamatwa na kufanya fujo huku akihoji aliyetoa taarifa zake na Makonda baada ya kupatiwa taarifa na kufika eneo la tukio na kuagiza awashiwe kamera za CCTV kuangalia kulichotokea, polisi waliohusika walionekana.
“Pia wapo askari waliomkamata mwananchi akiwa na mpenzi wake kwenye gari, wakawapiga picha za utupu na kuwalazimisha watoe sh. milioni tano ili wasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume sheria.
“Hatuwezi kuruhusu vitendo hivyo hapa mkoani. Ni lazima sheria na haki vitendeka kwa wananchi,” alisema Makonda.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa alisema wapo askari katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wanaoshirikiana na raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori ambao uchunguzi utakapokamilika wayashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya