Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Mtwara kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.
Agizo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Alisema Wilaya ya Tandahimba ina korosho za daraja la kwanza hivyo ni ajabu kuona korosho chafu na kuhoji zinatokea wapi.
Awali, Waziri Mkuu Majaliwa alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms alikotoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho kufunga mashine mpya na kuanza uzalishaji.