ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI, STANSLAUS NYONGO KATIKA MGODI WA HAMADÂ MINE SCALE ULIOPO WILAYA YA KWERWA, MKOA WA KAGERA
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mwenye Kaunda Suti-
mbele) na Ujumbe wake, baada ya kukagua mitambo inayotumika
kusaga mawe yenye Madini ya Bati (kulia) katika Mgodi wa Hamad
Mine Scale, uliopo eneo la Omukasheni, Wilaya ya Kyerwa, Mkoa
wa Kagera, Februari 28 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.
Naibu   Waziri   wa   Madini,  Stanslaus   Nyongo   (katikati),   akikagua
madini   ghafi   ya   Bati   (aliyoshika   mkononi)   na   kuzungumza   na
mmoja wa wamiliki wa mtambo wa kuchakata madini hayo, Hassan
Ibar   (kushoto),   alipotembelea   na   kuukagua   mtambo   huo
unaomilikiwa   na   Kampuni   ya   African   Top   Minerals,   wilayani
Kyerwa, Mkoa wa Kagera.
Mmoja wa wamiliki wa mtambo wa kuchenjua Madini ya Bati wa
TanzaPlus Minerals, Salim Mhando (kushoto), akimuonyesha Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kutoka kushoto), moja
ya mashine zinazotumika   kuchakata madini   hayo. Naibu Waziri
alitembelea   na   kukagua  mtambo   huo  uliopo  Nyaluzumbulwa
wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera
Madini ya Bati yaliyo ghafi.
Ujumbe wa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakikagua
shimo linalochimbwa Madini ya Bati katika Mgodi wa Hamad Mine
Scale,   uliopo   eneo   la   Omukasheni,   Wilaya   ya   Kyerwa   mkoani
Kagera.