Thursday, December 26, 2024
spot_img

Kiswahili chakwamisha kesi mahakakani

ARUSHA
Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) leo imeshindwa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Baraza la Serikali ya Kijiji cha Ololosokwan kwa sababu hati ya mashitaka imeandaliwa kwa Lugha ya Kiswahili.
Baraza la Serikali ya Kijiji cha Ololosokwan kilicho Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha limefungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania likiiomba EACJ iizuie Serikali kuwahamisha kwenye ardhi wanayoishi.
Shauri hilo liko mbele ya majaji watatu wa EACJ wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Monica Mugenyi ambaye aliahirisha shauri hilo kwa maelezo kuwa hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani, kwenye kesi namba 15 ya mwaka 2017 ina kasoro kwa sababu imeandikwa kwa Kiswahili badala ya Kingereza ambacho kinatambulika mahakamani hapo.
Aidha, alisema hati zimesainiwa na mawakili wawili tofauti hivyo mahakama imeshindwa kujua itumie hati gani ya mashtaka.
“Hati hizi zimesainiwa na mawaikili wawili tofauti, hakuna hati ya kiapo inayoonyesha ni halali na imefuata taratibu za kimahakama. Lakini pia mmeandika kwa Lugha ya Kiswahili wakati mnajua mahakama hii inatumia Lugha ya Kingereza.
“Kutokana na kasoro hizo tunalazimika kuahirisha kesi hii hadi hapo mtakaporekebisha kasoro mbalimbali zilizopo kwenye hati ya kiapo,” alisema Jaji Mugenyi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya