Thursday, December 26, 2024
spot_img

Mjukuu apanga mauaji ya babu yake kwa milioni moja


RUKWA

Mzee mwenye umri wa miaka 72 aliyefahamika kwa jina la Paul Kisiwa, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ng’ongo ameawa kwa kupigwa rungu kichwani.
Mzee huyo aliuawa Machi 3, mwaka huu majira ya jioni katika Kijiji cha Kifinga kilicho Kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando ambaye amesema watu sita akiwemo mjukuu wa mzee huyo wanashikiliwa na polisi.
Kamanda Kyando alisema mjuu wa mzee Kisiwa alikubali kuchukua sh. Milioni moja ili babu yake auawe.
Diwani wa Kata ya Mtowisa, Edger Malinyi naye amekaririwa akieleza kuwa mzee huyo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizikwa kimya kimya shambani kwake baada ya kuuawa.
“Taarifa za kupotea kwa Kisiwa zilianza kuzagaa. Ndugu na jirani zake wakishirikiana na polisi walianza kumtafuta, ilipofika Machi 8, mwaka huu walimbana mjukuu wake ambaye alikiri kupanga njama za kumuua babu yake baada ya kupewa Sh. 1,000,000.“Alipobanwa alieleza kuwa alipanga njama ya mauaji hayo na watu waliokuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na babu yake.
“Kwamba babu yake aliwakodishia watu hao shamba la ekari zaidi 15 kwa ajili ya shughuli za kilimo lakini baadaye aliwanyang’anya akaanza kulilima mwenyewe ndiyo wakakasirika wakaandaa mpango wa kumuua.
“Siku ya tukio la mauaji walimvamia akiwa shambani kwake, wakampiga na rungu kichwani ambalo lilimuua papo hapo.
“Baada ya kumuua, walichimba shimo shambani humo wakamzika ili kupoteza ushahidi. Mjukuu wake alionyesha mahali alipozikwa na polisi walipofukua waliukuta mwili wa mzee huyo,” alisema diwani huyo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya