Friday, December 27, 2024
spot_img

KENYA YAONDOA SHARTI LA USAFIRI WA ANGA KWA TANZANIA

 

NA CHARLES MULLINDA

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KCAA) imeondoa sharti la kuwekwa karantini kwa siku 14 kwa wasafiri wa ndege wanaoingia nchini humo wanaotokea Tanzania.

Taarifa ya kuondolewa kwa sharti hilo imetolewa Septemba 16 na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoeleza kuwa KCAA iliondoa sharti hilo Septemba 15.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali ya Tanzania nayo imeondoa amri ya kuzuia kampuni za ndege za Kenya kufanya safari zake nchini Tanzania.

“Kufuatia hatua hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeondoa amri ya kuzuia kampuni za ndege za Kenya ikiwemo Kenya Airways, Fly 540 Limited, Safarilink Aviation na AirKenya Express Limited kufanya safari zake nchini Tanzania.

” Kwa taarifa hii, sasa kampuni hizo za ndege za Kenya zimeruhusiwa kurejesha safari zake nchini mara moja na tayari Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya imejulishwa kuhusu uamuzi huo,” ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, katika taarifa yake hiyo, Johari ilieleza  kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuendesha na kusimamia shughuli za usafiri wa anga kwa kuzingatia misingi ya kimataifa ya usafiri wa anga kama ilivyoainishwa katika mkataba wa Chicago wa mwaka 1944 na mkataba wa usafiri wa anga baina ya nchi na nchi.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya