Friday, December 27, 2024
spot_img

SERIKALI YATUMIA BILIONI 25 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA MANISPAA MUSOMA

 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Musoma Mjini

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imetumia shilingi bilioni 25 kujenga na kukarabati barabarani na mitaa ya Manispaa ya Mji wa Musoma, Mkoa wa Mara.

Sambamba na hilo, serikali pia imeweka taa za barabarani zenye urefu wa kilomita 14 kupitia programu ya uboreshaji wa Miji (ULGSP) katika manispaa hiyo.

Hayo yameelezwa Septemba 21, 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa katika hotuba yake ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais John Pombe Magufuli.

Katika hotuba yake hiyo kwa wakazi wa Mji wa Musoma aliyoitoa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mara iliyoko Kata ya Nyamatare, Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu alisema hatua chanya zilizokwishachukuliwa ya serikali tangu mwaka 2015 ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 -2020.

Alisema ni lengo la serikali ni kuifanya miji yote ya Tanzania ukiwemo wa Musoma, usiku uwe mchana na mchana uendelee kuwa mchana.

“Shilingi bilioni 18.7 zimetumika kujenga kilomita 14 za barabara kwa kiwango cha lami na kuweka taa za barabarani kupitia programu ya uboreshaji wa miji (ULGSP) katika Manispaa ya Musoma na mradi umekamilika. Tunataka taa ziwake ili usiku uwe mchana na mchana uwe mchana.

“Kupitia road fund maintenance, kiasi kingine cha shilingi bilioni 6.6 kilitumika kwa ajili ya kufungua barabara mpya, kufanya matengenezo ya kawaida na matengenezo ya sehemu korofi na miradi yote imekamilika.

“Ninawasihi wana Musoma msisite kumpigia kura Dk. John Pombe Magufuli hata kama wewe ni mpenzi wa chama kingine kwa sababu yeye ndiye mleta maendeleo kwa nchi yetu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Akizungumzia miradi mingine iliyotekelezwa na serikali katika uhai wa miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano, Majaliwa alitaja uboreshaji wa huduma za upatikanaji maji katika Manispaa ya Musoma.

“Ili kuboresha huduma ya upatikanaji maji katika Manispaa ya Mji wa Musoma, shilingi bilioni 46 zilitolewa na serikali kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji safi wa Manispaa ya Mji wa Musoma ambao tayari umeanza kutoa huduma.

“Shilingi bilioni 18 zimetolewa kwa ajili ya mradi wa kusambaza maji Manispaa ya Musoma na vijiji vitatu vya Musoma Vijijini na Butiama. Kazi zinazofanywa sasa ni ujenzi wa tenki la Bharima lenye ujazo wa lita milioni tatu, ujenzi wa kituo cha kusukuma maji na ulazaji bomba la kusafirisha maji kwenda tenki la Bharima lenye kipenyo cha milimita 450 na urefu wa kilomita 1.56, alisema Majaliwa.

Alitaja kazi nyingine zilizofanyika kuwa ni ulazaji wa bomba la kusafirisha maji kutoka tenki la Bharima kwenda kwenye kaya za wananchi lenye kipenyo cha milimita 450 na urefu wa kilomita 7,058, ufungaji wa pampu tatu zenye uwezo wa kusukuma mita za ujazo 175 kwa saa, ununuzi  wa bomba za kusambaza maji kilomita 44.3 na ununuzi wa vifaa vya kutendea kazi.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya