Tuesday, December 24, 2024
spot_img

DC MURRO AMSHUKURU RAIS SAMIA KUMALIZA KERO YA MAJI IKUNGI


RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84 

MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji ya bomba wa rafiki Ikungi unaotarajiwa kuwanufaisha wakazi wa Kata za Unyahati na Ikungi

Murro aliweka jiwe hilo la msingi mapema mwezi huu ambapo thamani ya mradi ni Shilingi milioni 548 ambazo ni sehemu ya fedha za Uviko -19 

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi, Muro alisema mradi huo katika awamu ya kwanza utakuwa na maeneo nane ya umma ya kuchotea maji (vilula) na pia umetengenezwa ukiwa na uwezo wa kutoa huduma ya kuwaunganishia wananchi maji majumbani kutokana na miundombinu yake kupita kwenye maeneo ya makazi ya watu 

Muro alisema fedha tumika kujenga mradi huo ni sehemu ya fedha ambazo Rais Samia Suluhu Hassan alizitoa kwa Wilaya ya Ikungi ikiwa ni sehemu ya mapambano ya changamoto ya ugonjwa wa Uviko -19 na kwa sasa mradi umekamilika kwa asilimia 98 na vilula vyote vinatoa maji.

Alimshukuru Rais Samia kwa kuridhia Ikungi kupewa fedha hizo na kumuhakikisha kuwa zimesimamiwa kikamilifu mpaka mradi kukamilika na pia aliwapongeza watekelezaji wa mradi huo ambao ni Ruwasa Ikungi na Mkoa wa Singida.


Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya