RIPOTA PANORAMA
0711 46 49 84
MAKALA MAALUMU
MKOA wa Njombe upo katika kampeni ya kukuza sekta za viwanda na uwekezaji. Kampeni hiyo inakwenda kwa kasi na inaongozwa na viongozi vijana ambao mafanikio yao katika kuzipiga mbio za kuufungua mkoa huo ni makubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Sharifa Nabalangāanya ambaye katika kipindi kifupi cha kuiongoza halmashauri hiyo amesimika alama za maendeleo ambazo hatazifutika kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyokusudiwa huku akiwezesha kuikwamua ile iliyokuwa imekwama, sasa anawaita wawekezaji wa ndani na wa nje kwenda wilayani humo kuwekeza. Anasema Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ina fursa lukuki na milango ipo wazi kwa wawekezaji.
Wito huu anautoa baada ya kuandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji huku akiendelea kujenga miundombimu ambayo kwanza inawezesha ustawi wa haraka wa kiuchumi wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na pili mazingira rafiki ya uwekezaji kwa wawekezaji.
Katika mahojiano ya ana kwa ana aliyoyafanya hivi karibuni na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ustawi wa watu kiuchumi na kijamii pamoja na mambo mengine, Nabalangāanya anasema mafanikio anayoyapa katika utekelezaji wa majukumu yake yanachochewa na mamlaka iliyomteua kukanyaga naye unyayo mmoja katika kila hatua.
Nabalangāanya ambaye alianza mahojiano na Tanzania PANORAMA Blog kwa kulitambulisha eneo lake la utawala, kwa maneno yake mwenyewe, anasema; āHalmashauri ya Wilaya ya Njombe ni moja kati ya halmashauri sita zinazounda Mkoa wa Njombe, lakini pia ni moja kati ya halmashauri tatu zilizo katika Wilaya ya Njombe ambazo ni hii Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Halmashauri ya Mji Makambako na Halmashauri ya Mji Njombe.
āKihistoria, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ndiyo halmashauri mama ambayo imetoa halmashauri nyingine tatu ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Wagingāombe, Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri ya Mji Makambako.
āHalmashauri ya Wilaya ya Njombe ina kata 12. Kwenye eneo la utawala tuna madiwani wa kata 12 na tunao madiwani wa viti maalumu wanne hivyo tuna jumla ya madiwani 16 kwenye halmashauri yetu. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ina jimbo moja la uchaguzi ambalo ni Jimbo la Lupembe.Ā
āKwa upande wa watumishi tunao 1200 wa sekta zote. Kwa mwaka 2021 tulipata watumishi 34 na mwaka wa fedha ulioisha 2022 tulipata watumishi 37 na ninyi ni mashahidi wakati tunafunga mwaka wa fedha ulioisha wizara iliajiri watumishi wa sekta za afya na elimu.
āSisi Halmashauri ya Wilaya ya Njombe tumepata watumishi 37 wa kada ya elimu na afya na tayari tumeishawapangia vituo, Kwa hiyo tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu hivi sasa tumeongeza madarasa na kazi ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati mpya inaendelea hivyo watumishi hawa wapya wamekuja kwa wakati muafaka.
āTulikuwa na uhitaji wa watumishi kwa hiyo kupokea watumishi ndani ya muda mfupi tangu tumeanza tarehe moja mwezi wa saba ni kitu kikubwa sana kwetu. Tumuahidi Mheshimiwa Rais kuwa watumishi hao watafanya kazi kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria ili kuhakikisha malengo yake Mheshimiwa Rais hasa kwenye sekta hizi mbili yanatimia,ā anasema Nabalangāanya.
Sharifa Nabalang’anya |
Ā
Tanzania PANORAMA ilimuuliza Nabalangāanya kuhusu mwenendo wa hali ukuaji wa uchumi katika halmashauri yake naye bila kusita anasema; āHali ya uchumi kwa halmashauri yetu ya Wilaya ya Njombe inakua ukilinganisha na miaka ya nyuma.
āHapa, chanzo kikuu cha mapato kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ni mapato ya mazao ya bidhaa za misitu. Zaidi ya asilimia 70 ya mapato yetu ya ndani yanatokana na bidhaa za misitu. Wananchi wa Njombe kupitia mashamba ya miti uchumi wao unazidi kuimarika. Changamoto tunayoiona ni kuwa viwanda vilivyopo vinatumia miti mingi kwenye uzalishaji wa bidhaa, endepo kasi ya upandaji wa miti haitaendena na kasi ya ukataji tunaweza kupoteza miti mingi miaka inayokuja.
Shamba la miti |
Ā
āMimi na wenzangu hili tumeliona. Kuna wawekezaji wazuri wanatusaidia katika hili lakini na sisi lazima tubuni vyanzo vingine vya mapato ambavyo havitategemea bidhaa za miti. Baada ya kuliona hili nilikaa chini na wenzangu, tuliangalia tufanye nini kutoka kwenye kutegemea kwa kiasi kikubwa chanzo kimoja cha mapato, tukaangalia maeneo yetu tukaona tunaweza kutoka hapo kwa sababu tuna maeneo ambayo yanaweza kutuingizia fedha. Sasa tunataka kufanya uwekezaji wa maduka makubwa ya bidhaa (shopping mall) lakini pia tuna maeneo mazuri sana kwa ajili ya kujenga vituo vya mafuta.
“Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inamiliki ardhi Njombe Mjini na ardhi hiyo imepimwa na kutengwa kwa ajili ya matumizi ya uwekezaji wa kituo cha mafuta, kama nilivyosema maduka makubwa ya bidhaa (shopping malls).
“Eneo lililopo kwa ajili ya kituo cha mafuta ni square meter 2,602 na eneo kwa ajili ya shopping malls ni square meter 13,227. Viwanja hivi vyote vimepimwa na vina hati tayari kwa hiyo tunakaribisha wawekezaji ambao wataingia ubia na halmashauri na niwaambie maeneo haya yako eneo la kimkakati kibiashara.
āNa mpango wa halmashauri yetu kwa mwaka huu wa fedha ni kujenga vizimba kwa ajili ya kupangisha wafanyabiashara na hicho ni chanzo kimojawapo cha mapato ambacho halmashauri yetu imekibuni ambacho kitapunguza upungufu wa mapato yatokanayo na misitu.
āLakni pia tuna maeneo muhumu sana ya mawe. Tumekaa kama halmashauri na kukubaliana kuwa eneo lile la mawe ni muhimu sana kwa uchumi wa halmashauri yetu. Kwa hiyo tumeanza mkakati wa kutaka kuanza kulitumia eneo hilo kwa biashara ya kokoto.
“Tayari Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imefanikiwa kupata leseni mbili za madini ujenzi (kokoto) kutoka Wizara ya Madini. Eneo la kwanza ambalo tuna leseni tayari ni Kidegembye- Nyalive lenye ukubwa wa hekta 4.28 na eneo la pili ni Matembwe lenye ukubwa wa hekta 4.85, niendelee kutumia fursa hii kuwakaribisha sana wawezekaji kwa ajili ya uchimbaji wa kokoto. Mikoa ya nyanda za juu kusini ina miradi mingi mikubwa ambayo ina uhitaji mkubwa wa kokoto.
āKama tulivyosimama imara tutaendelea kusimama imara. Tunaamini ndani ya robo ya mwaka huu wa fedha tutaanza uzalishaji wa kokoto. Nasema tunaamini chanzo hiki kitatuongezea mapato kwenye halmashauri yetu.Ā
“Lakini pia tunatarajia kuweka mizani ya upimaji wa magari ya mizigo kama chanzo kingine cha mapato.Ā
āNimezungumzia vyanzo mbadala ambavyo kama halmashauri tuna vibuni lakini pia huku kwenye biashara ya miti tuna mikakati pia ya kuendeleza zao la miti na tayari halmashauri tuna shamba letu la miti, tuna ekeri 300, tumeamua kuwa na shamba letu la miti ili kukabiliana na tishio linalotunyemelea. Lakini pia tunakaribisha wawezekezaji kwa ajili ya kupanda miti, maeneo yapo yamepimwa na tumeyaweka kwenye investiment guide.
āKwa hiyo wale watakaokuja kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wasije kwa kusita sita, wajue kabisa kuwa tumekwishapanga ni maeneo gani kwa ajili ya kupanda miti. Maeneo yapo tayari.
āHapa nizungumzie pia upande wa sekta ya uwekezaji na viwanda kwa sababu ndiyo mahali pake. Tuna viwanda sita ambavyo tayari vimeishaanza kufanya kazi na viwanda hivyo sita vimetoa ajira kwa wananchi wetu 320. Kati ya hizo ajira 202 ni wanaume na 118 ni wanawake. Hawa ni wafanyakazi wa moja kwa moja kwenye hivyo viwanda.
āLakini kwa ajira ambazo siyo rasmi kwa maana kwamba wapo wanaozalisha bidhaa na kuzipeleka viwandani ni wengi sana. Kwa hiyo tunao wananchi wengi sana ambao wanajihusisha moja kwa moja na viwanda hivyo na hawa wananufaika moja kwa moja na viwanda hivyo.
āSisi kama halmashauri tumetenga maeneo yetu ya uwekezaji. Tumetenga maeneo ya kutosha kwenye Kata ya Mtwango ambako ni barabara kuu ya kutoka Iringa kwenye Songea. Tumetenga eneo la kuegesha magari ekari 15, stendi ekari 13.5, viwanda ekari 21 na ujenzi wa nyumba tumetenga ekari mbili na hizi tumeziweka kwa ajili ya wenye viwanda kama watahitaji kujenga nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wao. Watajenga wao au sisi kama halmashauri kwa kutumia mapato yetu ya ndani. Wawekezaji wanaokuja kwetu hatutaki waanze kukwamakwama ndiyo maana kila kitu tunakiweka katika mpangilio unaostahili.
āTumeona umuhimu wa viwanda na tunaendelea kutoa maeneo mengine ili wawekezaji watakapokuja wakikosa maeneo kutoka kwa wananchi waje kwetu halmashauri ambako maeneo yameishatengwa na yamepimwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda. Kwa hiyo nitumie tena fursa hii kuwakaribisha sana wawekezaji waje kwa wingi kwa sababu maeneo bado yapo lakini pia rasilimali watu ipo ya kutosha,ā anasema Nabalangāanya.
Shamba la parachichi |
Ā
Tanzania PANORAMA ilimuuliza Nabalangāanya kuhusu maendeleo ya kilimo katika halmashauri na hapa anaeleza; āKilimo hapa ndiyo pake hasa na ndiyo maana umepata shida kidogo kunipata kwa sababu ninalazimika kwenda site kwa wakulima wangu. Kwa upande wa kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe tuna mazao ya biashara na chakula. Mazao ambayo yanapatikana kwa wingi kwenye Halmashauri ya Wilaya Njombe kwanza ni zao la chai na kwenye zao hili la chai tayari kuna viwanda viwili ambavyo vinanunua chai kutoka kwa wananchi.
āViwanda hivi vinashughulika moja kwa moja na ununuzi wa zao la chai kutoka kwa wakulima, vinalichataka na kuuza chai ikiwa imeishaboreshwa thamani.
Shamba la chai |
Ā
āViwanda hivi vimeingia makubaliano na wakulima hivyo huwa vinawawezesha ili waweze kuzalisha mazao bora lakini pia soko la wakulima hao ni kwenye viwanda vyenyewe hivyo unaona jinsi sekta ya viwanda na uwekezaji inakuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kwenye halmashauri yetu lakini pia hata kuongeza mapato ya halmashauri.
āPia tuna zao la parachichi. Bado hatujapata kiwanda cha kuchakata zao la parachichi lakini wakulima wananufaika na zao hilo. Kuna makampuni ambayo yanakuja kununua moja kwa moja zao la parachichi kutoka kwa wakulima kwa hiyo kama nilivyosema mwanzo fursa bado zipo, maeneo ya kilimo cha zao la parachichi yapo.Ā
“Katika Kijiji cha Ikang’asi tuna hekta 5000 ambazo zinafaa kwa kilimo cha parachichi, chai na mazao ya miti. Katika Kijiji cha Mtwango tuna ekari 400Ā ambazo zinafaa kwa kilimo cha ngano, alizeti, mahindi na viazi. Mtwango ni kata ambayo ipo barabara kuu ya kutoka Iringa kwenda Songea. Niendelee kuwaomba wawekezaji waje Wilaya ya Njombe kwa ajili ya kilimo cha zao la parachichi na mazao mengine niliyoyataja.
āMazao niliyoyataja yanalimwa na kustawi vizuri sana katika Halmashauri ya Wilaya ya NjombeĀ na nimeishazungumzia miti ambako halmashauri tuna ekari 300 tulizopanda miti lakini maeneo kwa ajili ya kilimo cha miti bado yapo ya kutosha.
āKatika eneo hili nako nawakaribisha wawekezaji na wadau mbalimbali wakaribie Wilaya ya Njombe kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo na viwanda kwa ajili ya kuchakata mazao ya miti.
āArdhi ni nzuri, hali ya hewa ni nzuri na miti inastawi vizuri. Yaani kila hatua hata kwenye maeneo ya vijijini utaona hali ya hewa inavyowezesha miti kustawi.
āNa kama nilivyosema kwa upande wa mazao ya chakula katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe tuna viazi na ngano lakini pia tuna matunda. Hali ya Njombe wengi tunaiona kama ni ya baridi maeneo yote lakini kuna kata mbili zinapakana na Mkoa wa Morogoro hali yake inaruhusu sana ulimaji wa matunda na tunda linalolimwa sana ni nanasi.
Shamba la nanasi |
Ā
āKwa ujumla Halmashauri ya Wilaya ya Njombe katika upande wa kilimo tunakwenda vizuri sana na wananchi wamekuwa wakinufaika kwa kila aina ya kilimo wanachojishughulisha nacho. Watanzania wenye mitaji yao wanaotaka kufanya kilimo biashara mimi nawakaribisha Wilaya ya Njombe, nawahakikishia hawatajuta bali watanufaika sana sana,ā anasema Nabalangāanya.
Mkurugenzi Mtendaji huyo pia anaitumia fusra hiyo kuzungumzia kwa ufupi utekeleaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri yake kwa kueleza kuwa; āSasa nizungumzie miradi ya maendeleo hasa fedha zilizotoka Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.
āNianze na mwaka wa fedha wa 2020/2021 ambao Serikali Kuu ilituletea Shilingi bilioni 4.2 lakini kwa mwaka wa fedha 2021/2022 tumepokea kutoka Serikali Kuu, Shilingi bilioni 7.2 ambazo zimewezesha kuboresha sekta ya afya na tumepokea Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya Ikondo, ujenzi unaendelea.
āBaadhi ya fedha za miradi ambazo tumepokea ni Shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa majengo manne ya hospitali ya Halmashauri, Shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya jengo la utawala, Shilingi milioni 560 kwa ajili ya madarasa ya Uviko; na pia tumepokea Shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kichiwa. Mpaka hapa nadhani hata wewe mwandishi unaweza kuona jinsi Serikali Kuu ilivyo serious kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake. Hivyo vituo vya afya viwili vinavyojengwa vitasaidia kutatua tatizo la upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo hayo.
āTulipokuwa tunaibua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Ikondo, wananchi hawakuamini mpaka viongozi wa dini wa eneo hilo waliamua kufanya ibada maalumu ili wazo la kuweka kituo cha afya pale liwe wazo ambalo halitakwama. Hivyo unaona jinsi ambavyo wananchi wamepelekewa huduma muhimu kwenye maeneo yao, huduma ambazo walikuwa wanazikosa kwa muda mrefu.
āHizi fedha nyingi tunazopokea kutoka Serikali Kuu zimetuwezesha pia sisi halmashauri kuwekeza fedha za kutosha kwenye miradi ya maendeleo. Tuna kituo cha afya tunachokijenga Kata ya Mtwango kutoka fedha za mapato yetu ya ndani. Kituo hiki kina majengo nane, nafikiri ni kituo cha mfano kwenye halmashauri zote Tanzania na kituo hiki kikipata majengo mawili mengine kinaweza kufikia hadhi ya kuwa hospitali. Haya ukitaka kupata picha halisi ufike siteukaone kazi inayofanyika siyo kuongelea ofisini humu.
āLakini bila Serikali Kuu kutuletea fedha nyingi za miradi ya maendeleo, sisi kama halmashauri kupitia fedha za mapato ya ndani tusingeweza kuwa na uwezo wa kujenga kituo kikubwa cha namna hii. Lakini pia inawezesha hata fedha tulizopeleka kwenye uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa maana ya mikopo kuwa cha kutosha hasa, tusingeweza kutoa kwa kiwango kikubwa ambacho tumekitoa mwaka huu bila Serikali Kuu kuweka mkono wake.
āMwaka wa fedha ulioisha tumetoa Shilingi bilioni 1.04 za asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaĀ vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Jumla ya vikundi 125 vimenufaika. Hii haijawahi kutokea.
āKwa hiyo kama halmashauri inapokea fedha nyingi kutoka Serikali Kuu, nayo kupitia mapato ya ndani inakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi, vikundi vinanufaika na miradi ya kiuchumi vinavyoifanya inaleta tija na hali ya uchumi wa halmashauri yetu inakua ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Sharifa Nabalang’anya |
Ā
āMimi kwa heshima kubwa, nitumie fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu, Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini vijana na wanawake katika nafasi zake za uteuzi. Kikubwa tunachomuahidi ni kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili tusimuangushe. Lakini pia nimpongeze sana kwa kazi anayoifanyia nchi yetu, ndani ya muda mfupi tumeona mabadiliko makubwa kwenye sekta mbalimbali. Tunazidi kumuombea afya njema.
“Sasa nawashukuru sana ninyi watu wa PANORAMA kwa muda huu mlionipa, sasa naelekea shamba. Mtakapokuja tena tutakwenda kuongelea siteili muwe mnaona kazi inavyoendelea, asanteni sana,ā anamalizia Nabalangāanya kisha anasimama tayari kwa safari ya kwenda vijijini kuhamasisha kilimo.