Wednesday, December 25, 2024
spot_img

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATAKA UDHIBITI MIMBA TANDAHIMBA

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka kuwepo udhibiti wa mimba za utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.

Akizungumza jana na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, alisema ni lazima viongozi wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike wa wilaya hiyo dhidi ya mimba ili waendelee na masomo.

“Kwa nini kila mwaka mimba Tandahimba zinaongezeka, viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukulia hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.

“Lazima wahusika wote wakamatwe wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria kwa sababu wanaharibu elimu ya mtoto wa kike,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu kutowafungia ndani na badala yake wawapeleke shule.

“Watakaobainika kuwafungia ndani watoto wenye mahitaji maalumu wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu wanawakosesha haki ya kupata elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya