Home HABARI CCM YAMJIBU HECHE KUHUSU HALI YA UPATIKANAJI MAFUTA NCHINI

CCM YAMJIBU HECHE KUHUSU HALI YA UPATIKANAJI MAFUTA NCHINI

0

CCM yamjibu Heche kuhusu mafuta

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amewataka wanasiasa kuacha upotoshaji kuhusu sababu za kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Kauli hiyo inakuja kufuatia tamko la Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, aliyedai kuwa pamoja na sababu nyingine, uwepo wa tozo na kodi 18 kwenye lita ya mafuta umechangia kupanda kwa bei ya nishati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 7, 2026 mjini Dodoma, Kihongosi amesema hakuna Serikali au chama kinachofurahia changamoto zinazowakumba wananchi wake.

Amesema kupanda kwa bei ya mafuta ni changamoto ya kimataifa, inayochangiwa na mivutano ya kisiasa na kijeshi inayoendelea duniani, ikiwemo kati ya Marekani, Israel na Iran.

“Zinapotokea changamoto, tusiweke siasa katika maisha ya watu. Kuna baadhi ya viongozi wanazungumzia mambo ambayo hawana uelewa nayo. Ni vyema wakajielimisha zaidi, hususan katika masuala ya uchumi,” amesema Kihongosi.

Katika hatua nyingine, amewataka wananchi kuwa na subira akieleza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo, kama ilivyofanya wakati wa majanga mengine.

Amekumbusha kuwa hata kipindi cha vita kati ya Urusi na Ukraine, Serikali ilitoa ruzuku ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version