Sunday, November 23, 2025
spot_img

KAMISHNA KUJI ATAKA UBUNIFU NA UFANISI TIL

RIPOTA PANORAMA

Arusha

KAMISHNA wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Musa Nassoro Kuji amewataka watumishi wa Kampuni Tanzu ya TANAPA, TANAPA Investment Ltd (TIL) kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa ufanisi.

Amesema wafanyakazi wa TIL wapanaswa kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika utoaji wa huduma za ukandarasi ndani na nje ya shirika.

Akizungumza jana na watumishi wa TIL, Jijini Arusha alisema mwenendo wa ufanyaji kazi wa kampuni hiyo ni mzuri na kazi lilizofanya ni za kuzipigiwa mfano kwa ubora.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya. Ukarabati wa barabara ya Hifadhi ya Taifa Arusha, ukarabati wa kiwango cha changarawe wa baadhi ya barabara za Jijini Arusha, ukarabati wa kipande cha barabara ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kazi nyingine ambazo mmefanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

Kamishna Mussa Nassoro Kuji akiwa katika kikao na maofisa wa TIL.

“Pokeeni pongezi kutoka Bodi ya Wadhamini ya Shirika. Bodi imenituma niwaeleze kuwa inayo matarajio makubwa sana kutoka kwenu, hivyo msiwaangushe.

“Endeleeni kufanya kazi kwa weledi, bidii, nidhamu, kujituma, ushirikiano, upendo na mshikamano ili muweze kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa TIL” alisema Kamishna Kuji.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TIL, Mhandisi Dkt.Richard Matolo alimshukuru Kamishna Kuji kwa kutenga muda wake kuzungumza na watumishi wa kampuni hiyo na kuahidi kuchapa kazi kwa ari na kasi zaidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na bodi ya wadhamini kupitia kampuni hiyo.

TIL ni Kampuni tanzu ya TANAPA; ilianzishwa mwaka 2019 lengo likiwa kutekeleza miradi ya shirika na kuwa kitega uchumi cha TANAPA.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya