Sunday, September 7, 2025
spot_img

MAPINDUZI MAMLAKA YA BANDARI

RIPOTA PANORAMA

KUNA mapinduzi Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Ni mapinduzi makubwa ya utoaji huduma, gharama za meli kusubiri nangani kuhudumiwa na ya makusanyo ya mapato.

Taarifa rasmi ya TPA kuhusu mwenendo wa utoaji huduma na ukusanyaji mapato kwa mwaka 2024/2025 ambayo Tanzania PANORAMA imeona, inaonyesha kuwepo kwa mapinduzi hayo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka 2024/2025 yamefanyika mapinduzi makubwa ya muda wa meli za makasha kusubiri nangani. Muda wa meli kusubiri nangani umeondolewa, sasa meli zinazowasili katika Bandari ya Dar es Salaam zinakwenda moja kwa moja gatini.  

Hilo lilielezwa kwanza na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akiwasilisha  hotuba ya wizara hiyo bungeni, Dodoma kuhusu mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2035/2026.

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Alisema hali hiyo imepunguza wastani wa meli kusubiri nangani kutoka siku 46 za awali hadi siku saba.

Pia taarifa zinaonyesha kwa mwaka 2024/2025, uhudumiaji wa makasha nao umeboreshwa ambapo sasa idadi ya makasha yaliyohudumiwa imeongezeka hadi kufikia 686,515.

Takwimu hizi ni kwa kipindi cha Julai, 2024 hadi Februari, 2025 zilikilinganishwa na takwimu za kipindi kama hicho kwa mwaka 2023/2024 ambapo yalihudumiwa makasha 670,724.  

Waziri Profesa Mbarawa katika hotuba yake bungeni alisema uwekezaji uliofanyika katika gati namba saba, umechochea kufikiwa kwa mafanikio hayo ambako idadi ya makasha yaliyohudumiwa katika eneo hilo yaliongezeka hadi kufikia 160,286 kutoka 122,339 katika kipindi hicho.

Meli kubwa ya mizigo ikienda kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mapinduzi mengine yaliyofanyika TPA ni kuimarika kwa utoaji huduma, ambapo kwa mwaka 2024/2025 muda wa meli kusubiri nangani kuhudumiwa umepungua kutoka siku 30 hadi siku tatu na kwa meli za mafuta pia muda wa kusubiri kuhudumiwa umepungua kutoka siku 10 hadi siku tatu.

Upakuaji wa makasha Bandari ya Dar es Saalaam.

Waziri Profesa Mbarawa alilieleza Bunge kuwa mapinduzi hayo yameiwezesha TPA kukusanya mapato wastani wa shilingi trilioni moja kwa mwezi kwa mwaka 2024/2025, kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 kwa mwezi kwa mwaka 2023/2024.

Aidha, kwamba, mapato yanayokusanywa kutokana na ushuru wa forodha yameongezeka kutoka shilingi trilioni 9.35 mwaka 2023/2024 hadi shilingi trilioni 9.86; kwa takwimu za Februari, 2025.

Haina shaka hata kidogo kuwa mapinduzi haya ya kimafanikio yamefanyika baada ya Serikali kuchukua maamuzi magumu ya kuimarisha utendaji kazi wa Bandari za Tanzania.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya