Sunday, September 7, 2025
spot_img

RAIS KABILA ADAIWA SI MTOTO WA RAIS KABILA

Kinshasa DRC

BAADHI ya maafisa wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), waibua madai kuwa rais wa mstaafu wa nchi hiyo, Joseph Kabila si mtoto halisi wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Desire Kabila.

Madai hayo yamedakwa na baadhi ya vyombo vya habari vya DRC na kuanza kuyaripotiwa kwa uzito wa juu, jambo ambalo limeibua mjadala miongoni mwa jamii ya wacongo.

Taarifa zilizopatikana kutoka Kinshasa, DRC zimeeleza kuwa kuibuka kwa madai hayo kutoka kwa viongozi wa juu wa Serikali ya Kinshasa kumeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakionyesha kushangazwa na madai hayo.

Tayari wakili wa Rais Mstaafu Joseph Kabila, anayemwakilisha kwenye kesi ya uhaini na kushirikiana na kundi la waasi wa AFC/M 23   inayomkabili mahakamani, amelaani madai hayo akieleza kuwa ni udhalilishaji.

Wakili huyo amesema mke wa Hayati Laurent Kabila, rais wa zamani wa DRC aliyeuawawa kwa kupigwa risasi, Sifa Kabila, anapaswa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu walioibua madai hayo.

“Familia ya Joseph Kabila na hasa mama Sifa Kabila (mama yake Joseph Kabila na mke wa Laurent Kabila) ina haki za kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Jamhuri na mwandishi wa taarifa hizo za kashfa.

“Kisheria madai yoyote lazima yaongozwe na ushahidi wa wazi, sahihi na unaoweza kuthibitishwa,” alisema wakili huo.

Haya yanajiri wakati Rais Mstaafu Kabila akikabiliwa na mashtaka mahakamani ya uhaini na kushirikiana na kundi la waasi la AFC/ M 23 ambako mwezi uliopita, waendesha mashtaka wa kijeshi wa DRC waliiomba mahakama imuhukumu kifo na mali zake zote zitaifishwe.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya