Monday, September 1, 2025
spot_img

CHAKULA CHANUNULIWA KWA TAKA ZA PLASTIKI

MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA

TAKA za plastiki sasa zinatumika kununua chakula kwenye migahawa nchini India.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya kimataifa, manunuzi ya chakula kwa kutumia taka za plastiki yanafanyika zaidi katika Jiji la Ambikapur, lililopo Jimbo la Chhattisgarh, nchini India.

Ripoti zinaeleza kuwa watu wenye njaa wamekuwa wakipata mlo kamili bila kulipa pesa, badala yake wanawakabidhi wauza chakula mifuko ya taka za plastiki walizokusanya majalalani.

Moja wa migahawa inayotoa huduma hiyo unafahamika kwa jina la ‘Garbage Cafe’ au ‘mgahawa wa taka’ ambao ulizinduliwa mwaka 2019 ukiwa na kauli mbiu isemayo ‘taka zaidi ladha bora zaidi ya chakula.’

Inaelezwa kuwa mfuko wa kilo moja ya taka za plastiki ambazo ni chapa na vifungashio  unanunua mlo kamili wa mchana ukiwa na wali, mboga aina mbili, chapati, saladi na achari huku mfuko wenye nusu kilo ya taka za plastiki unanunua kifungua kinywa kama chai, sambusa na andazi.

“Jiji la Ambikapur lilijipatia sifa ya kuwa jiji zaidi nchini India mwaka 2016 kwa sababu ya biashara hiyo kwani taka zinakusanywa kwa kiwango kikubwa. Dampo lenye ukubwa wa ekari 16 limegeuzwa kuwa bustani ya takataka na mfumo unaofahamika kama ‘zero waste’ umezinduliwa.

“Taka za plastiki zinazokusanywa kwenye mgahwa huo hupelekwa kwenye vituo maalumu vya ukusanyaji taka na kuna vituo 20 vya ukusanyaji taka huku vikundi zaidi ya 60 vikiwa vinajihusisha na biashara ya uchakata taka kwa ajili ya kutumika tena.

“Vituo hivi vimeajiri wanawake wapatao 480 wanaotambulika kwa jina la ‘Wachhata didis,’ likiwa na maana, ‘ndugu wa usafi’ na kazi yao ni kukusanya taka nyumba kwa nyumba,” inaeleza sehemu ya taarifa iliyopo kwenye Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Utafiti wa wanahabari umeonyesha kuwa taka za plastiki zinazokusanywa huchakatwa na kugeuzwa chembechembe kwa ajili ya ujenzi wa barabara na taka mbichi huchimbiwa chini kuwa mbolea.

Inaelezwa kuwa takriban tani 50,000 za taka kavu ambazo ni plastiki, karatasi, chuma na taka za elekitroniki zimekusanywa katika kipindi cha miaka tisa kwenye Jimbo la Chhatisgarh.

Hata hivyo, ripoti zinaeleza kuwa ingawa waokota taka wanapewa vifaa vya kujikinga, wengi wao hawana kinga dhidi ya maambukizi ya taka hatarishi hivyo uwepo wa wasiwasi wa afya zao ni mkubwa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya