MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi ya Taifa ya Mpira wa Wavu unatarajiwa kuanza Julai 25, mwaka huu, kwenye viwanja wa Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Panorama, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF), Magoti Mtani, alisema maandalizi ya ligi hiyo yanaendelea vizuri.
Mtani alisema timu zitakazopata nafasi ya kushiriki ligi hiyo zitatakiwa kujisajili kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Alisema msimu huu ligi hiyo itakuwa ikionyeshwa moja kwa moja kupitia Azam Media na Youtube, hivyo klabu zinatakiwa ‘kujibradi’ ili timu zao ziweze kuonyesha kiwango ambazo kitawavuta mashabiki wengi viwanjani.
Bingwa mtetezi wa ligi hiyo ni timu ya wanawake na wanaume ya magereza.