Wednesday, July 16, 2025
spot_img

KOCHA ALIYEKUFUZWA YANGA, AOMBA KURUDI

KOCHA mkuu wa zamani wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet, ni miongoni mwa makocha watano walioomba kibarua cha kuifundisha timu hiyo, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Saintfiet aliwahi kuifundisha Yanga kwa siku 80 kabla ya kufukuzwa Julai 4, 2012, baada ya kufungwa mabao 3-0 na timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Kabla ya kutimuliwa kwake, Saintfiet alianza msimu vibaya baada ya kupata suluhu na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, licha ya kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa, Santifiet ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya Mali, imeelezwa kwamba kocha huyo amewasilisha wasifu wake (CV), akiomba kurithi mikoba ya Miloud Hamdi aliyeachana na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu wa 2024/2025 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chanzo chetu kiliwataja makocha wengine waliojitokeza kuomba kurithi mikoba ya Hamdi ni pamoja na Rulani Mokwene wa Mamelodi Sundowan ya Afrika Kusini na julien Chevalier wa Asec ya Ivory Coast

Hata hivyo, Panorama ilimtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, kwa lengo la kujua uweli kuhusu hilo, lakini simu yake iliita bila majibu,

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya