Wednesday, July 16, 2025
spot_img

KIKOSI CHA KUOGELEA CHATAJWA HADHARANI

KIKOSI cha Tanzania cha Kuogelea kimetajwa hadharani kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya ‘Africa Acquatics’, Kanda ya 3, iliyopangwa kufanyika Oktoba 16-19, mwaka huu.

Akizungumza na Panorama, Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Amina Mfaume, alisema wametangaza kikosi cha awali wakiwamo waogeleaji chipukizi na wakongwe kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo.

Amina alisema katika kikosi hicho wameitwa waogeleaji wenye umri wa kuanzia miaka 17 kwa lengo la kupata kikosi bora endelevu cha Taifa.

Alisema timu ya ufundi ya TSA, imepanga waogeleaji wataanza mazoezi Agosti mwaka huu, chini ya makocha wa Taifa, wakiongozwa na kocha mkuu Alexander Mwaipasa.

Makocha wengine watakaokinoa kikosi hicho ni pamoja na Agnes Kimimba, Kanisi Mabena na Ally Msaizi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya