Bao la kiungo mshambuliaji wa Mali, Saratou Traore, lilitosha kuipa ushindi dhidi ya kikosi cha wanawake wa Tanzania, ‘Twiga Stars’ katika michezo wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) uliochezwa jana kwenye Uwanja Berkane, mjini Morocco.
Saratou alifunga bao pekee dakika ya nyongeza ya kipindi cha kwanza kwa shuti Kali baada ya mabeki wa Twigs Stars kushindwa kuokoa mpira wa hatari wa adhabu kwenye lango lao.
Katika michezo huo, Mali walianza kucheza kwa kasi wakitumia nguvu kubwa kuhakikisha wanapata bao dhidi ya wapinzani wao Twiga Stars..
Hats hivyo, Twiga Stars walikosa nafasi nyingi za kufunga kutokana na ubutu wa washambuliaji wao