Tuesday, July 8, 2025
spot_img

MTIBWA SUGAR KULETA KOCHA MPYA

UONGOZI wa klabu ya Mtibwa Sugar, umesema unatarajia kumwajiri kocha mkuu mpya ili aweze kukifundisha kikosi chao cha msimu ujao.

Mtibwa Sugar wamerejea Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushuka daraja msimu wa 2022/2023 kutokana na kufanya vibaya michezo yao.

Akizungumza na Panorama, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema kwa sasa wapo katika harakati ya kuboresha benchi la ufundi ambalo litakabidhiwa majukumu ya kukifundisha kikosi chao.

Kifaru alisema wamepokea wasifu (CV) za makocha wengi wakiwamo wazawa na wa kigeni ambao wameomba kazi ya kukinoa kikosi chao cha msimu ujao.

Alisema kwa sasa wanaendelea kupitia wasifu wa makocha hao ili mmoja wao ambaye atakuwa na sifa zaidi ya ukocha atakuwa kocha wa timu hiyo.

Pia alisema bàada ya kukamilisha mchakato wa kupata kocha mkuu watakaa na benchi la ufundi kwa lengo la kuweka mkakati wa pamoja katika suala nzima la usajili wa wachezaji wapya.

”Tunarajia kocha akija tutakaa naye na kujenga mkakati wa pamoja wa kuiwezesha timu kufanya vizuri msimu ujao,” alisema Kifaru.

Kifaru alisema malengo ya klabu hiyo ni kufanya vizuri baada ya kuikosa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya