Friday, July 4, 2025
spot_img

MO DEWJI AVUNJA KAMATI YA USAJILI WA WACHEZAJI SIMBA

Baada ya timu ya Simba kushindwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kikao cha viongozi wa klabu hiyo kimepitisha uamuzi wa kuvunja kamati ya usajili wa wachezaji kwa kushindwa kutimiza malengo yao.

Kikao hicho kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam, chini ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji maarufu kwa jina la MO, kilitathimini mwenendo mzima wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na kubaini kwamba kamati ya usajili ilishindwa kusajili wachezaji wenye viwango.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya kikao hicho kilisema kwa sasa kamati itakuwa chini ya bosi mwenywe MO Dewji.

Mpaka tunaingia chumba cha habari juhudi za kumpata Mkuu wa kitengo cha Habari ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya msimbazi kariakoo Ahmed Ally simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa ili kuweza kuthibitibisha taarifa hizi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya