Friday, July 4, 2025
spot_img

KOROSHO QUEENS KWENDA MAFICHONI JULAI 25

TIMU ya wasichana ya korosho Queens ya Mtwara, inatarajia kuingia kambini kujiandaa na Ligi ya Taifa ya Mpira wa Wavu (TVNL), iliyopangwa kuanza Julai 25, mwaka huu, kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa wachezaji wa kikosi hicho kimepewa mapumziko ya wiki moja baada ya kutoka katika mashindano ya UMISETA yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Iringa na wataingia kambini kuanzia Julai 8 hadi 22, mwaka huu.

Kocha Mkuu wa Korosho Queens, Enock Ankyooo, alisema kikosi hicho kitaweka kambi katika Shule ya Sekondari ya Mkapa iliyopo Mangata Nanyumbu.

Alisema walianza maandalizi ya awali yakiwamo kwa wachezaji kushiriki mashindano ya Umoja wa Michezo ,Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yalifanyika mkoani Iringa.

“Baada ya kurejea katika michezo ya shule UMITASHUMTA na UMISETA tumetoa mapumziko ya muda mfupi ya wiki moja wakasalimie familia zao na tuweze kuingia kambini kujiandaa na ligi iliyopo mbele yetu,” alisema Akyoo.

Akyoo alisema ataendelea kuwekeza kwa vijana wazawa kwa kuthamini vipaji vyao ili viweze kuonekana.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya