KOCHA mpya wa Azam, Florent Ibenge, amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Salum Abdallah, ‘ Fei Toto’ ataendelea kukipiga katika kikosi hicho.
Ibenge ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ( DRC), amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha timu ya Azam akitokea All Hilal ya Sudan.
Hata hivyo, ujio wa Ibenge kwenye kikosi hicho cha Azam unaonekana kuzimaliza Yanga na Simba ambazo zilikuwa zinawania saini ya Fei Toto kwa ajili ya msimu ujao.
Ibenge ameonyesha nia ya kuendelea kufanya kazi na kiungo huyo, kutokana na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti.